Dalasini (kwa Kiingereza cinnamon) ni aina ya kiungo chenye harufu nzuri kilichokaushwa kutoka katika gome la ndani la spishi 6 za miti za jenasi Cinnamomum katika familia Lauraceae inayoitwa mdalasini.
Gome linaweza kukatwa katika vipande, kuviringishwa katika "vijiti" au kusagwa kuwa ungaunga.
Kiungo hiki hutumika katika mapishi ili kuongeza ladha na kuleta harufu nzuri katika chakula. Pia hutumika kutengenezea chai ya dalasini.
Dalasini ni kiambato kikubwa cha michanganyiko mbalimbali ya viungo kama vile aina kadhaa za masala, k.m. masala ya chai na garam masala.
*1. Hutibu matatizo ya kibofu
*2. Hutibu kansa.
*3. Hutibu matatizo ya uzazi.
*4. Hutibu tumbo.
*5. Hutibu mafua.
*6. Hutibu magonjwa ya ngozi.
*7. Huondoa harufu mbaya mdomoni.
*8. Husaidia kupunguza unene.
*9. Huondoa chunusi.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Dalasini, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.