Triti (pia tritiumu, ing.
Tritium) ni isotopi nururifu ya hidrojeni yenye masi atomia 3.016. Triti ina protoni moja na nyutroni mbili. Kiini cha hidrojeni ya kawaida haina nyutroni bali protoni moja tu. Alama ya Triti ni 3H bali T hutumiwa pia.
Katika mazingira asilia triti hutokea kwa kiasi kidogo sana kutokana na mnururisho kutoka anga-nje unapopasua atomu za nitrojeni hewani. Triti nu nururifu na nusumaisha yake ni mnamo miaka 8 tu hivyo inapotea haraka. Triti inatengenezwa katika tanuri nyuklia kwa matumizi mbalimbali.
Kuna isotopi nyingine ya hidrojeni inayoitwa duteri yenye nyutroni moja.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Triti, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.