Mchele ni punje za mpunga zilizokobolewa baada ya mavuno na kabla ya kupika.
Kama hazijakobolewa na ziko bado katika ganda ni mpunga. Kama zimepikwa huitwa wali.
Watu wengi hununua mchele dukani. Ni punje kavu kabisa zinazokaa muda mrefu hata mwaka bila kuharibika kama hakuna unyevu wala wadudu.
Penye kilimo cha mpunga watu wananunua pia magunia wakikoboa kiasi kile wanachohitaji kwa kipindi.
Mpunga una faida hauathiriki sana na wadudu, lakini mchele uko hatarini kuliwa.
Mchele uliovunjika huuzwa bei nafuu.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mchele, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.