Marselino na Petro ni Wakristo wa karne ya 3 waliouawa mwaka 304 kwa ajili ya imani yao mjini Roma.
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.
Kuhusu maisha yao, hatuna habari nyingi za hakika. Marselino alikuwa padri, na Petro mzinguaji. Wote wawili waliuawa kwa kukatwa kichwa katika dhuluma ya Kaisari Diokletian dhidi ya Wakristo wa Dola la Roma.
Simulizi la kifodini chao la Papa Damas I ndilo chanzo cha kale zaidi juu yao. Damas alieleza kwamba alipata habari kutoka kwa muuaji wao ambaye baadaye alijiunga na Kanisa
Kwake tumepata kujua kwamba walipopelekwa kwenye vichaka vya miiba ili kuuawa, walilazimishwa kujichimbia makaburi yao, ili maiti wasionekane na yeyote, lakini Lusila alifaulu kuwazika kwa heshima mjini kwenye barabara inayoitwa Labicana, ambapo baadaye lilijengwa basilika maarufu.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Marselino na Petro, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.