Makari wa Aleksandria (300 hivi - 395) alikuwa mmonaki maarufu katika jangwa la Nitria.
Alikuwa kijana zaidi kidogo kuliko Makari Mkuu, ndiyo sababu anaitwa pengine Makari Kijana.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Januari au 1 Mei.
Mzaliwa wa Aleksandria, alikuwa mfanyabiashara hadi umri wa miaka 40, alipobatizwa na kwenda kuishi jangwani.
Baada ya miaka kadhaa, alipewa upadrisho na kufanywa priori wa monasteri fulani, katika mlima Nitria.
Mwaka 335, Makari alikwenda kuishi peke yake katika jangwa la el-Natroun akiwa mkuu wa wakaapweke zaidi ya elfu tano.
Miujiza mingi inasimuliwa kuwa ilifanywa kwa maombezi yake.
Alipofikia umri wa miaka 73 Makari alipelekwa uhamishoni na Kaisari Valens, pamoja na Makari Mkuu wakaishi katika kisiwa fulani ambacho walifaulu kukiinjilisha.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Makari wa Aleksandria, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.