Kipi Sijasikia ni wimbo uliotoka tarehe 15 Septemba, 2014 kutungwa na kuimbwa na msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania, Professor Jay.
Katika wimbo, ameshirikishwa mwimbaji wa Bongo Flava - afisa mtendaji mkuu wa WCB, Diamond Platnumz. Wimbo umetayarishwa na P. Funk wa Bongo Records. Wiki ambayo wimbo huu umetoka, Jay alitoka nyimbo tatu kwa siku tatu mfululizo. Ya kwanza "Chafu Tatu", ya pili "Kipi Sijasikia" na ya tatu "Sauti ya Ghetto". Wimbo una madongo kibao dhidi ya wale wanaomsema vibaya maisha ya Jay. Video ya muziki huu imeongozwa na Adam Juma wa Next Level Production. Walionekana katika video ni pamoja na Rommy Jones, DJ Choka, P. Funk, Kulwa Kikumba (Dude) na wengine wengi. Jay anaimba kwa uchungu mno dhidi ya wenye visonoko na ngebe juu yake.
“Kipi Sijasikia” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Kava la Kipi Sijasikia | |||||
Single ya Professor Jay akiwa na Diamond Platnumz | |||||
Imetolewa | 15 Septemba, 2014 | ||||
Muundo | Upakuzi wa kidijitali | ||||
Imerekodiwa | 2014 | ||||
Aina | Hip hop | ||||
Urefu | 4:05 | ||||
Studio | Bongo Records | ||||
Mtunzi | Professor Jay | ||||
Mtayarishaji | P. Funk | ||||
Mwenendo wa single za Professor Jay akiwa na Diamond Platnumz | |||||
|
Ubunifu pekee katika wimbo huu ni kwenye video. Inaanza anakamatwa, anapelekwa mahakani, anashinda na mwishoni anaonekana akiwa na marafiki zake wanakula raha za dunia kwa raha mustarehe kabisa licha ya magumu aliyopitia hapo awali.
Sijasikia Video katika YouTube
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Kipi Sijasikia, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.