Edward Estlin Cummings (kwa kifupi E.
E. Cummings; 14 Oktoba 1894 - 3 Septemba 1962) alikuwa mshairi na mwandishi mashuhuri kutoka Marekani. Kwa jumla aliandika na kuchapisha mashairi, riwaya na tamthilia mia tisa. Vile vile, Cummings alijulikana sana kama mchoraji wa picha kadhaa zilizovutia.
Mashairi ya Cummings yaligusia sana masuala ya mapenzi na mazingira - alipenda sana kuandika juu ya majira ya kuchipua. Mashairi yake yalipata umaarufu kwa sababu hayakuakifishwa kama ilivyo kawaida.
Watalaamu wengi wanaamini kuwa Cummings alikuwa mmojawapo wa washairi waliojulikana sana kule Marekani katika karne ya 20. Mashairi aliyoandika Cummings, na ambayo yanajulikana sana, ni kama: "In Just Spring", "A Man Who Had Fallen Amongst Thieves", "The Cambridge Ladies" na "Buffalo Bill".
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Edward Cummings kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Edward Cummings, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.