Spishi >1000; 36 katika Afrika ya Mashariki:
Chungu | ||||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mfanyakazi wa chungu (Camponotus cinctellus) | ||||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||||
Chungu spishi kubwa za sisimizi katika jenasi Camponotus ya nusufamilia Formicinae zinazotokea katika misitu ya mabara yote isipokuwa Antaktiki. Kwa sababu hujenga makoloni yao ndani ya mbao, huitwa “carpenter ants” (sisimizi seremala) kwa Kiingereza. Ingawa spishi hizi sio kali sana, zinaweza kung'ata vinususi na kupuliza asidi fomi kwenye jeraha, ambayo huleta uchungu kali.
Chungu ni spishi kubwa za sisimizi ambao hujenga makao yao katika mbao nyevu zinazooza. Koloni lina malkia (wakati mwingine kadhaa), madume wapevu kadhaa na matabaka matatu ya wafanyakazi: wadogo, wa kati na wakubwa. Malkia wanaweza kuwa na urefu wa hadi sm 2.5, huku madume wakiwa na ukubwa takriban nusu. Wafanyakazi wakubwa huwa wakubwa kuliko madume kwa kawaida. Wafanyakazi wadogo wanaweza kuwa wadogo kama sm 0.75 na wa kati wako kati bila shaka. Ingawa spishi nyingi na matabaka mengi ni nyeusi, zinaweza kuwa kahawia au mchanganyiko wa nyeusi, kijivu na kahawia. Spishi fulani hubeba nywele nyeupe, njano au kahawianyekundu.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Chungu (sisimizi), which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.