Bikira Maria wa Mlima Karmeli ni jina linalopewa Bikira Maria kama msimamizi wa Wakarmeli.
Wa kwanza wao walikuwa wakaapweke walioishi mwishoni mwa karne ya 12 na mwanzoni mwa karne ya 13 katika Nchi Takatifu juu ya Mlima Karmeli, ambapo zamani Nabii Eliya alirudisha Waisraeli kumuabudu Mungu aliye hai.
Katikati ya makazi yao walijenga kikanisa kwa heshima ya Bikira Maria, msimamizi wao.
Tangu karne ya 15 watu wamemheshimu kwa jina hilo hasa kwa kuvaa skapulari ya kahawia inayosemekana Maria alimpa Mkarmeli Simoni Stock (1165-1265).
Kumbukumbu katika liturujia inafanyika tarehe 16 Julai.
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bikira Maria wa Mlima Karmeli kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Bikira Maria wa Mlima Karmeli, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.