Aspaja ni ugonjwa wa akili.
Inaonyeshwa na shida katika kuwasiliana na wengine na kuanzisha uhusiano wa kijamii.
Watu walioathiriwa wana ugumu wa kuelewa hisia; wana uwezo wa kupata hisia kama vile pendo, lakini kwa njia tofauti.
Watu wenye ugonjwa wa Aspaja mara nyingi ni watu wenye akili sana. Wamejaliwa kumbukumbu ya ajabu na mantiki ndio msingi wa hoja zao. Pia wana ufahamu mkubwa na ujuzi mzuri wa uchambuzi.
Tunaona katika ugonjwa huu kuharibika kwa mawasiliano na wengine. Mtu aliye na dalili hii ana ugumu wa kuamua maana ya sura ya uso, maana ya sauti, na maana ya ishara za mwili za watu wengine. Ni lazima ajifunze na haichukui kiotomatiki kama watu wengine wanavyofanya. Anatumia akili na mantiki yake kubaini mambo huku wengine wakielewa kiasili bila kufikiria.
Ugonjwa husababisha wasiwasi mkubwa wa ndani.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Aspaja, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.