Karibu kuchangia kwenye Wikipedia ya Kiswahili! Tayari ni Wikipedia kubwa ya Kiafrika - pamoja na lugha ya Afrikaans.
Unaombwa kujiandikisha kwanza ingawa si lazima, lakini inasaidia! Maelezo yake ni hapa: Wiki: Mwongozo (Kujisajili).
Kabla ya kuanza panga makala yako. Wikipedia ni kamusi elezo.
Kuna njia mbili za kuhariri makala kwenye wikipedia.
Maelezo yanayofuata yanahusu njia ya kawaida.
Ukitaka kubadili, kusahihisha au kuhariri makala, ubonyeze "hariri chanzo" kule juu katika ukurasa wowote.
Usiandike makala bila viungo, kwa sababu bila hivi maandishi yako hayatapatikana kwa mtu yeyote yatabaki siri yako tu!
Njia rahisi ya kuanzisha ni kutumia viungo vilivyopo bila makala. Haya yanaonekana kwa rangi nyekundu. Ukiona neno lenye rangi nyekundu maana yake ni ya kwamba mwandishi aliona inafaa kueleza jambo lile lakini hakuna makala bado. Ukibonyeza hapo utafungua ukurasa mpya na unaweza kuanza kuandika!
Ukitaka kuanzisha makala mpya kabisa, andika jina katika dirisha la "tafuta" upande wa kushoto kando la dirisha. Gonga "Nenda" na wikipedia inatafuta makala kama ipo tayari kwa jina hili au la karibu. Kama haipo inaweza kuonyesha orodha ya makala mbalimbali ambako jina hili latokea - au hutaona orodha kama jina bado ni geni kabisa.
Lakini kwa namna yeyote utaona mstari "Create the page "(JINA)" on this wiki!" (JINA) ina rangi nyekundu. Bonyeza hapa na ukurasa mpya wa kuanzisha makala unajitokeza!
Kwa mfano, ukitaka kuanzisha ukurasa kuhusu "Plovdiv",
Ukitaka kujua ufanye nini ili kusaidia kuboresha kamusi elezo hii, angalia Wiki: Makala za msingi za kamusi elezo utaona majina kwa rangi nyekundu haya ni makala yanyokosekana bonyeza tu na kuanza! Unasaidia pia ukiandika makala juu ya vichwa vya viungo vyekundu vinavyopatikana katika makala mengi kidogo.
Makala iwe fupi au ndefu lakini sentensi za kwanza ni muhimu hasa.
Makala ndefu bila mpangilio haivuti. Inasaidia sana ukiingiza vichwa. Hii ni rahisi! Utumie alama za = mbele na nyuma ya mstari wa kichwa.
==Kichwa kikubwa==
===Kichwa kidogo===
Ukitaka kutumia picha iliyopo katika Wikipedia ya lugha nyingine kuna njia mbili:
Hii ni jambo la kujaribu! Fungua makala katika lugha nyingine yenye picha inayotakiwa, bonyeza "edit", nakili yote pamoja na mabano.
Kwa mfano: [[Image:Europe CD 3 036.jpg|right|300px|thumb|View over Paris from the Eiffel Tower]])
Hapo unahitaji kubadilisha Maelezo ambayo ni maneno ya mwisho kati ya | na ]]. Andika elezo kwa Kiswahili kwa mfano "Paris inayvoonekana kutoka mnara wa Eifel". Ukitaka kubadilisha ukubwa unabadilisha namba mbele ya "px". 200 px itakuwa ndogo zaidi, 100 px ndogo sana, 400 px kubwa zaidi - wakati mwingine tayari kubwa mno. Jaribu kwa kubonyeza hapo chini kabisa "Mandhari ya mabadilisho". Ukiona picha - sawa. Usipoona picha: haipo mahali inapopatikana. Jaribu nyjia ya pili!
a) hifadhi picha kwenye kompyuta unayotumia (kwa muda tu - baada ya kupakia unaweza kuifuta mara moja).
b) Jiandikishe kwa jina lako katika wikipedia ya Kiswahili. (bofya juu kulia, andika jina unalotumia)
c) chini kushoto utapata kiungo kinachoitwa "Pakia faili" (chini ya andiko "vifaa"). Bofya kiungo hicho.
d) Katika ukarasa ujao, unabofya kando la dirisha ndogo "Search" na kuteua faili ya picha kwenye kompyuta yako. Kwenye "summary" pakia anwani ya picha kwa mfano "http://en.wikipedia.org/wiki/Image:Europe_CD_3_036.jpg" kwa picha ya Paris. Halafu bofya "Upload file", na picha itakuwemo Wikipedia ya Kiswahili.
Unaweza kutumia picha kwa kuandika [[Image:jina_la_picha.jpg]].
Mara nyingi inatokea kwamba majina mawili yanafaa kwa makala fulani. Ikiwa hivi, lazima tuamue makala ipatikane chini ya jina gani. Lakini tunaweza kuelekeza kutoka jina jingine kwa jina sahihi la makala, ili watu waipate makala rahisi zaidi.
Ili kuelekeza kutoka jina moja kwenda jina sahihi la makala, tumia
Unaweza kuangalia mfano huu: Abunuwasi.
Usisahau kuunganisha makala yako na jamii au category. Jamii ni kama orodha ya makala zote chini ya kichwa fulani.
Kwa mfano makala zote kuhusu nchi za Afrika zimeorodheshwa katika jamii "Jamii:Nchi za Afrika". Tafuta jamii inayoweza kufaa (tazama ukurasa wa Mwanzo). Wengine watasaidia kupanga makala yako ikionekana jamii nyingine inafaa zaidi. Kwa maelezo zaidi angalia Msaada:Jamii.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Wiki:Msaada wa kuanzisha makala, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.