Mkutano wa Kimataifa juu ya Haki za Binadamu ulifanywa na Umoja wa Mataifa mjini Vienna nchini Austria tarehe 14 mpaka 25 Juni 1993.
Ulikuwa mkutano wa kwanza wa haki za binadamu uliyofanyika tangu kumalizika kwa vita baridi vya Dunia.
Matokeo ya mkutano huo yalikuwa Azimio la Vienna na Mpango wa Utendaji.
Ingawa Umoja wa Mataifa ulikuwa umeshughulika kwa muda mrefu katika uwanja wa haki za binadamu, mkutano wa Vienna ulikuwa mkutano wa pili wa kuzingatia haki za kibinadamu, na wa kwanza ulikuwa Mkutano wa Kimataifa wa Haki za Binadamu uliofanyika Teheran, Iran , wakati wa Aprili-Mei 1968 kuashiria kumbukumbu ya miaka ishirini ya Azimio la ulimwengu la Haki za Binadamu. .
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mkutano wa Kimataifa juu ya Haki za Binadamu, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.