Mama wa Kanisa (kwa Kilatini: Mater Ecclesiae) ni jina la heshima ambalo Bikira Maria amepewa rasmi na Papa Paulo VI tarehe 21 Novemba 1964 wakati wa Mtaguso wa pili wa Vatikano.
Jina hilo lilitumiwa kwanza na Ambrosi wa Milano katika karne ya 4 halafu na Papa Benedikto XIV mwaka 1748, tena na Papa Leo XIII mwaka 1885.
Limeingizwa na Papa Yohane Paulo II katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki, hatimaye na Papa Fransisko katika kalenda ya liturujia ya Kanisa la Kilatini siku inayofuata Pentekoste.
Kabla ya hayo yote, sanaa ya Kikristo ilikuwa imezoea kumchora Bikira Maria kati ya Mitume wakati wa kushukiwa na Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste kama ilivyosimuliwa na Mwinjili Luka (Mdo 1-2).
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mama wa Kanisa, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.