Juvénal Habyarimana (8 Machi 1937 – 6 Aprili 1994) alikuwa rais wa pili wa Rwanda.
Alitawala karibu mikaka 20 kuanzia 1973 hadi 1994. Alitoka katika jumuiya ya Wahutu akaongoza serikali iliyolenga kuzuia kurudi kwenye mamlaka kwa Watutsi ambao ni kundi kubwa la pili nchini Rwanda.
Juvénal Habyarimana | |
Habyarimana in 1980 | |
Rais wa Rwanda wa pili | |
---|---|
Muda wa Utawala 5 Julai 1973 – 6 Aprili 1994 | |
mtangulizi | Grégoire Kayibanda |
aliyemfuata | Théodore Sindikubwabo |
tarehe ya kuzaliwa | Ruanda-Urundi | Machi 8, 1937
tarehe ya kufa | Aprili 6, 1994 (umri 57) Kigali, Rwanda |
utaifa | Rwanda |
chama | MRND |
ndoa | Agathe Habyarimana |
dini | Kanisa Katoliki |
Kwa lugha ya Kinyarwanda aliitwa "Kinani" inayomaanisha "asiyeshindwa". Habyarimana alitawala kama dikteta na watazamaji hamini alidanganya katika kila uchaguzi aliosimamia.
Alikufa tarehe 6 Aprili 1994 wakati ndege yake ilipigwa na makombora aliporejea Kigali kutoka majadiliano ya amani pale Dar es Salaam. Ndege hii ilimbeba pia rais wa Burundi, Cyprien Ntaryamira. Haijulikana kama makombora yalifyatuliwa na Wahutu wakali waliochukia siasa yake au na wanamgambo Watutsi wa RPF waliokuwa wamefika karibu na Kigali wakati ule.
Tukio hili lilichukuliwa na Wahutu wakali kama ishara ya kushambulia Watutsi kote Rwanda pamoja na Wahutu wasioshikamana nao na hivyo kuanzisha mauaji ya kimbari ya Rwanda. Katika kipindi cha siku 100 zilizofuata, idadi ya Warwanda 800,000 hadi milioni 1 waliuawa.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Juvenal Habyarimana, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.