Jennifer Anne Doudna (amezaliwa Februari 19, 1964) ni mkemia wa Marekani ambaye amefanya kazi za mwanzo katika kugundua teknolojia ya uhariri jeni kwa kutumia Njia ya ''CRISPR'' pamoja na michango mingine ya muhimu kwenye tasnia za biokemia na jenetiki.
Doudna ni mmoja wa wanawake wa kwanza kupokea tuzo ya Nobel katika sayansi. Alipokea Tuzo ya Nobel katika Kemia mwaka 2020 pamoja na Emmanuelle Charpentier "kwa ajili ya kutafiti mbinu ya uhariri wa jenomu."
Doudna ni professa wa chansela ya Li Ka Shing katika idara ya kemia na idara ya biolojia ya molekuli na seli katika Chuo Kikuu cha California, Berkeley. Pia amekuwa Mtafiti katika Taasisi ya Matibabu ya Howard Hughes tangu mwaka 1997.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Jennifer Doudna, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.