Irene Pancras Uwoya (alizaliwa 18 Desemba 1988) ni mwigizaji na mwongozaji wa filamu, mwanamitindo wa zamani na mjasiriamali kutoka nchini Tanzania.
Irene pia alishiriki mashindano ya "Miss Tanzania" na kushika nafasi ya tano mwaka 2006/2007
Irene Pancras Uwoya | |
---|---|
Amezaliwa | 18 Desemba 1988 Dodoma, Tanzania |
Jina lingine | Oprah |
Kazi yake | Mwigizaji Mwanamitindo |
Miaka ya kazi | 2007 |
Ndoa | Cyprus Hamad (mtalaka), Dogo Janja (mtalaka) |
Watoto | 1 |
Tovuti rasmi |
Alifahamika sana kwa uhusika wa "Oprah" (2008) alioshiriki na Steven Kanumba na Vincent Kigosi. Baadhi ya filamu alizocheza ni pamoja na Uliyemchokoza Kaja, Figo, Rosemary, Snitch, The Return of Omega na Money.
Uwoya alianza shule ya msingi Mlimwa kisha akahamia Shule ya Bunge iliyopo Dar-es-Salaam kwa ajili ya elimu ya upili. Baadaye akaenda Greenville jijini Kampala, Uganda.
Kwenye mwezi Oktoba 2017, habari zilitapakaa katika mitandao mbalimbali nchini Tanzania kuwa Uwoya ameolewa na Dogo Janja - msanii wa hip-hop Tanzania. Siku kadhaa mbele kupitia ukurasa wake wa Instagram Uwoya alithibitisha kuolewa na Dogo Janja.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Irene Uwoya kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Irene Uwoya, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.