Adrian Atiman (Tindirma, Sudan ya Kifaransa, leo Mali, 1866 hivi - Karema, mkoa wa Katavi, 24 Aprili 1956) alikuwa katekista na daktari wa Kiafrika mmisionari nchini Tanzania.
Msonghai, alikombolewa na Wamisionari wa Afrika kutoka utumwa huko Metlili, kusini mwa Algeria.
Baada ya kusomeshwa hadi Ulaya aliishi na kufanya kazi katika misheni ya Karema kuanzia mwaka 1889 hadi kifo chake akiheshimiwa na wote kwa huduma zake zilizomfikisha hata vijiji vya mbali.
Aliacha mke na mtoto mmoja, padri Joseph, pamoja na masimulizi ya maisha yake.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Adrian Atiman, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.