Ruiru ni mji wa Kaunti ya Kiambu, ipatikanayo katikati ya Kenya.
Ruiru | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Kaunti | Kiambu |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 238,858 |
Mji huu uko katika umbali wa takribani kilomita 3 kutoka katika Mpaka wa Nairobi.
Una eneo la km2 292 na umezungukwa na mashamba ya Kahawa. Ruiru ni mmoja kati ya miji inayotambulika zaidi nchini Kenya, ambao unaweza kufikika kwa urahisi kupitia barabara au reli.
Mji huu umekuwa na ongezeko la idadi ya watu, kutokana na uhaba wa nyumba mjini Nairobi.
Mwaka 2009 ulikuwa na wakazi 238,858.
Hata hivyo, mji huu umeng'ang'ana kuwatosheleza wakazi wake.
Wengi wa wakazi wa Ruiru ni wafanyabiashara wenye asili ya Kikuyu.
Mji huu pia una matawi ya benki kadhaa kama vile Benki ya Equity, Benki ya Family, Benki ya Cooperative na Benki ya Barclays.
Pia kuna viwanda mbalimbali katika mji huo.
1°08′56″S 36°57′25″E / 1.14889°S 36.95694°E
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ruiru kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Ruiru, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.