Mlamani

Walamani (kwa Kiingereza: herbivores) ni wanyama wanaokula mimea pekee au hasa.

Maumbile yao yanalingana na chakula cha kimea na yanahusu hasa mdomo au viungo vya kukatakata chakula halafu matumbo yaani viungo vya kumeng’enya chakula. Viungo hivi ni tofauti baina ya walamani na walanyama.

Mlamani
Kulungu mwekundu na ndama wawili wakila majani
Mlamani
Kiwavi anakula

Walamani wanashirikiana mara nyingi na bakteria maalumu wanaoishi katika matumbo na kuzalisha vimeng'enya vinavyowawezesha kuvunja kwa mfano selulosi ya mimea.

Spishi nyingi za walamani hula hasa aina fulani za mimea. Mfano ni panda mkubwa anayekubali majani ya mwanzi pekee.

Kuna walamani wanaokula wakati mwingine pia protini, kwa mfano mayai. Mlanyasi kama ng'ombe hula pia wadudu waliopo kwenye nyasi.

Wanyama wanaoweza kula nyama pamoja na majani wakifanya hivyo mara kwa mara hawahesabiwi kati ya walamani bali huitwa walavyote.

Kuwepo kwa walamani ni msingi kwa kuwepo kwa walanyama. Kiekolojia walamani hutumia nishati iliyokusanywa ndani ya mimea kwa njia ya usanisinuru halafu wanawindwa na walanyama.

Marejeo

Mlamani  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mlamani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

ChakulaKiingerezaKiungoMaumbileMdomoMimeaTumboUmeng'enyaji wa chakulaWalanyamaWanyama

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

WazaramoUfahamuWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiTafsiriIsraeli ya KaleUrusiBaraza la mawaziri TanzaniaMkoa wa RukwaUkristo barani AfrikaSanaaThe MizMalawiDr. Ellie V.DEe Mungu Nguvu YetuOrodha ya Marais wa BurundiSikukuuFasihi ya KiswahiliMbiu ya PasakaSarufiMnyamaHekaya za AbunuwasiKombe la Dunia la FIFASayansiMsumbijiHarusiNuru InyangeteSilabiAgano JipyaUandishi wa ripotiSabatoTamthiliaOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaMarekani27 MachiUti wa mgongoKiswahiliElimuUshogaShengTanganyika (ziwa)Upinde wa mvuaKonsonantiNgeli za nominoChuraPaul MakondaPandaDawa za mfadhaikoZuhura YunusMariooShomari KapombeMkoa wa ArushaHarmonizeMbuniTaasisi ya Taaluma za KiswahiliMuundo wa inshaUchekiKemikaliKimondo cha MboziInjili ya YohaneOrodha ya nchi kufuatana na wakaziOrodha ya vitabu vya BibliaYesuTesistosteroniBunge la TanzaniaMaji kujaa na kupwaKisaweCristiano RonaldoSimbaBustani ya EdeniFananiHaikuMkoa wa NjombeAbby ChamsFaraja KottaOrodha ya vyama vya siasa TanzaniaJustin Bieber🡆 More