Nusukipenyo ya Jua (ing.
solar radius) ni nusu ya kipenyo cha Jua letu na hivyo sawa na umbali wa kilomita 696.342 au mara 109 nusukipenyo cha Dunia.
Umbali huu hutumiwa kama kizio katika sayansi ya astronomia kwa kutaja ukubwa wa magimba kwenye anga-nje hasa nyota.
Mfano wa matumizi yake ni mfumo wa Dunia na Mwezi: umbali kati ya Dunia na Mwezi ni takriban kilomita 384.400 au asilimia 55 za nusukipenyo ya Jua. Kama Jua lingechukua nafasi ya Dunia njia ya obiti ya Mwezi ingekuwa ndani ya Jua lenyewe.
Kipenyo na nusukipenyo ya Jua hubadilika kidogo kufuatana na sehemu ya kukipima kwa sababu Jua si tufe kamili. Kwa sababu hiyo kuna ufafanuzi wa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia wa kuhesabu nusukipenyo ya Jua kuwa na mita 6.957×108 au kilomita 695.700 .
Alama yake ni R☉ ambapo "R" inamaanisha "radius" na ☉ ni ishara ya Jua.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Nusukipenyo ya Jua, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.