Fungunyota

Fungunyota (kwa Kiingereza star cluster) ni idadi ya nyota zinazokaa karibu katika anga-nje.

Zinashikamana kwa nguvu ya graviti. Fungunyota maarufu linaloonekana kwa macho ni Kilimia.

Fungunyota
Fungunyota la Kilimia
Fungunyota
Fungunyota tufe lenye jina la kisayansi Messier2 jinsi linavyoonekana kwa darubini

Kwa kutumia mitambo ya kisasa wataalamu wa astronomia wamekuta mafungunyota maelfu kadhaa lakini nyingi hazionekani kwa macho matupu au yanaonekana kama nyota ya kawaida tu.

Fungunyota ni tofauti na kundinyota. Katika kundinyota watu wanajumuisha nyota zinazoonekana kukaa karibu na kuwa na umbo maalumu wakitazama anga kwa macho, lakini hali halisi nyota hizo hazina uhusiano kati yao wala hazipo pamoja. Nyingine zipo karibu zaidi na Dunia na nyingine zipo mbali mno. Kinyume chake fungunyota ni kundi la nyota zilizopo karibu hali halisi.

Kwa jumla kuna aina mbili za fungunyota:

  • fungunyota la kawaida ambako kwa kawaida idadi ya nyota haizidi mamia kadhaa. Kilimia ni fungunyota la aina hii lakini ni kati ya nyota sita hadi tisa tu zinazoonekana kwa macho matupu kutegemeana na hali ya anga.
  • fungunyota tufe lina idadi ya nyota maelfu hadi milioni zinazokaa karibu kama tufe kubwa. Chache zao zinaonekana kama nyota kwa macho lakini nyingi zimeonekana tu tangu kupatikana kwa mitambo ya utazamaji ya kisasa.


Marejeo

Viungo vya nje

Fungunyota 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
Fungunyota  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fungunyota kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Anga-njeGravitiIdadiKiingerezaKilimiaMachoNyotaen:star cluster

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Jumuiya ya MadolaMuhammadAsiaGhanaJinaUhuru wa TanganyikaPesaUandishi wa barua ya simuMizimuWimboChuiBoris JohnsonKilatiniVielezi vya idadiAgano la KaleMkondo wa umemeMohammed Gulam DewjiUislamuSiafuWanyakyusaMsumbijiShikamooUkoloniMr. BlueIsimuAbedi Amani KarumeInshaAfrika Mashariki 1800-1845MkungaHoma ya mafuaRedioMtende (mti)Faraja KottaKatekisimu ya Kanisa KatolikiHaikuAC MilanMbeya (mji)HarusiMike TysonAgano JipyaMungu ibariki AfrikaAunt EzekielClatous ChamaMkoa wa ArushaKito (madini)Kishazi tegemeziOrodha ya wanamuziki wa AfrikaYouTubeOrodha ya shule nchini TanzaniaJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaMkanda wa jeshiSerikaliNomino za dhahaniaSemiMuundo wa inshaTanganyika (ziwa)MalariaJackie ChanKipaimaraNevaViwakilishi vya pekeeUbuntuOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaAdhuhuriKiraiOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaKaswendeDeuterokanoniMwanamkeWahayaUgonjwa wa kuharaMajira ya mvuaOsimosisiUjima🡆 More