Wingu

Wingu ni matone madogo ya maji yanayoelea pamoja katika angahewa juu ya ardhi.

Mawingu ni mahali ambako mvua na theluji hutoka.

Wingu
Mawingu angani

Kutokea kwa mawingu

Asili yake ni mvuke wa maji unaotokea wakati jua linabadilisha maji kuwa gesi ya H²O; mvuke unapanda juu kwa sababu ni nyepesi kuliko hewa. Baada ya kupanda kiasi cha kutosha hufikia umbali penye baridi na mvuke unatonesha kuwa matone madogo ya maji. Kama wingu ni juu sana baridi inasababisha mvuke kuwa fuwele za barafu au theluji.

Mvuke unahitaji viini kwa kutonesha. Viini hivi ni aina zote za vumbi iliyoko hewani. Mvuke uliopo hewani unaanza kutonesha kwenye vipande hivi vidogo sawa na mvuke katika chumba cha jikoni au bafuni unaotonesha kwenye kioo cha dirisha au ukutani.

Kuelea kwa mawingu na kunyesha kwa mvua

Matone ndani ya wingu yanaweza kuelea angani kwa muda mrefu kama ni madogo. Mara nyingi matone madogo huwa na kipenyo cha milimita 0.001 hadi 0.015 hivyo ni nyepesi na mwendo wa kuanguka ni polepole. Hali halisi hayaanguki kwa sababu mawingu hutokea sehemu penye upepo wa kupanda juu na mwendo wa upepo huzidi au kulingana na mwendo wa kuanguka kutokana na graviti.

Lakini matone yana mwelekeo wa kuungana na kuwa makubwa zaidi. Yanaweza kufikia kipenyo cha milimita 1-3 na kuwa mazito zaidi. Sasa uvutano wa graviti unapita mwendo wa upepo na matone yanaanza kuanguka chini kama usimbishaji.

Wingu 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:

Tags:

AngahewaMajiMvuaTheluji

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Kamusi ya Kiswahili sanifuVichekeshoTarafaUtandawaziNabii IsayaKishazi tegemeziKata (maana)Samia Suluhu HassanPunyetoInjili ya MathayoUendelevuRiwayaAfrika KusiniShabuItikadi kaliMillard AyoBloguKanisa KatolikiYesuVita vya KageraSimu za mikononiMohammed Gulam DewjiMilaKhadija KopaHistoria ya TanzaniaAli Hassan MwinyiOrodha ya Magavana wa TanganyikaUandishi wa barua ya simuMkoa wa SimiyuJoyce Lazaro NdalichakoVidonge vya majiraIsimuNdoaBaruaTungo sentensiKidoleMajeshi ya Ulinzi ya KenyaUwanja wa Taifa (Tanzania)Mwanzo (Biblia)NgonjeraVipera vya semiReptiliaMaskiniAfrika ya MasharikiAdolf MkendaMnyoo-matumbo MkubwaSikioVita ya Maji MajiHussein KaziOrodha ya nchi kufuatana na wakaziNusuirabuKitenzi kishirikishiPalestinaZana za kilimoDolar ya MarekaniYvonne Chaka ChakaHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoBiashara ya watumwaVieleziNyangumiVivumishi ya kuulizaTanzaniaLa LigaMkoa wa ArushaSan Jose, CaliforniaUsultani wa ZanzibarFonimuMafua ya kawaidaNamba za simu TanzaniaBurundiHistoria ya WapareChumaHuduma ya ujumbe mfupiTohara🡆 More