Wakopti

Wakopti (au Wakhufti) ni Wakristo asili wa Misri, ambao wanafuata madhehebu ya pekee katika kundi la Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki na wanaunda kundi kubwa zaidi la wakazi wasio Waislamu katika nchi hiyo .

Wakopti
Msalaba wa Kikopti wenye maandishi asili yanayosema: 'Yesu Kristo, Mwana wa Mungu'.
Wakopti
Picha ya Kikopti ya Mwinjili Marko, anayehesabiwa kuwa mwanzilishi wa Kanisa la Misri.
Wakopti
Rais Nasser wa Misri akipokea ujumbe wa Maaskofu wa Kikopti (1965).
Wakopti
Kanisa la Mt. Marko huko Bellaire, Texas, Marekani. Wakopti milioni 4 wanaishi nje ya Misri.

Patriarki wao ni Papa Tawadros II, akiwa na makao makuu jijini Cairo.

Historia

Aina hiyo ya Ukristo ilikuwa anaongoza kabisa kati ya dini za Misri kuanzia karne ya 4 hadi karne ya 6 B.K., lakini baada ya uvamizi wa Waarabu (641), Uislamu ulizidi kuenea kwa njia mbalimbali.

Hata hivyo, Wakopti wanabaki asilimia 10-20 ya Wamisri wote, isipokuwa wanazungumza Kiarabu, si Kikopti tena, ambacho kinatumika tu katika liturujia.

Wakopti wengine wana ushirika kamili na Kanisa Katoliki, na wengine tena ni Waprotestanti.

Jina Kopti linatokana na Kigiriki Αἰγύπτιος, "Egyuptios", yaani "Mmisri".

Kati ya watakatifu muhimu zaidi wa Kikopti kuna mmonaki Antoni Abati na maaskofu Atanasi wa Aleksandria na Sirili wa Aleksandria.

Mchango mkubwa zaidi walioutoa ni kuanzisha umonaki na kutetea umungu wa Yesu Kristo pamoja na usahihi wa kumuita Bikira Maria "Mama wa Mungu".

Kutoka Misri, Ukristo wa aina hiyo ulienea tangu zamani hasa Sudan, Ethiopia na Eritrea.

Siku hizi Wakopti wengi wanazidi kuhamia nchi nyingine, hasa za Magharibi.

Jumla yao imekadiriwa kuwa milioni 18-22.

Tanbihi

Marejeo

  • Capuani, Massimo et al. Christian Egypt: Coptic Art and Monuments Through Two Millennia (2002) excerpt and text search
  • Courbage, Youssef and Phillipe Fargues. Judy Mabro (Translator) Christians and Jews Under Islam, 1997.
  • Ibrahim, Vivian. The Copts of Egypt: The Challenges of Modernisation and Identity (I.B. Tauris, distributed by Palgrave Macmillan; 2011) 258 pages; examines historical relations between Coptic Christians and the Egyptian state and describes factionalism and activism in the community.
  • Kamil, Jill. Coptic Egypt: History and a Guide. Revised Ed. American University in Cairo Press, 1990.
  • Meinardus, Otto Friedrich August. Two Thousand Years of Coptic Christianity (2010)
  • Thomas, Martyn, ed. (2006). Copts in Egypt: A Christian Minority Under Siege : Papers Presented at the First International Coptic Symposium, Zurich, September 23–25, 2004. Vandenhoeck & Ruprecht. 
  • Van Doorn-Harder, Nelly. "Finding a Platform: Studying the Copts in the 19th and 20th Centuries" International Journal of Middle East Studies (Aug 2010) 42#3 pp 479–482. Historiography

Viungo vya nje

Tags:

Wakopti HistoriaWakopti TanbihiWakopti MarejeoWakopti Viungo vya njeWakoptiMadhehebuMakanisa ya Kiorthodoksi ya MasharikiMisriWaislamuWakristo

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Joseph Sinde WariobaClatous Chama23 ApriliMbogaMkoa wa Unguja Mjini MagharibiUKUTAKilatiniAfrika Mashariki 1800-1845BurundiGoogleKiunguliaSheriaGudeKlamidiaKwame NkrumahWanyihaTenziMaziwa ya mamaMwakaHifadhi ya mazingiraPasakaMkoa wa Dar es SalaamHekalu la YerusalemuHali ya hewaHifadhi ya SerengetiViwakilishi vya sifaFarasiKanisa la Kiinjili la Kilutheri TanzaniaPichaZakaJapaniKanuni ya Imani ya MitumeKamusi za KiswahiliMkoa wa MorogoroMwanzo (Biblia)Ukomeshaji wa Biashara ya WatumwaMadiniMkoa wa ShinyangaKanaliNamba za simu TanzaniaMsamiatiNuruNywilaOrodha ya matajiri wakubwa WaafrikaNgono zembeSaratani ya mlango wa kizaziRose MhandoHistoria ya ZanzibarDubuTiktokSaidi Salim BakhresaDolar ya MarekaniNgonjeraBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiKidole gumbaZama za ChumaWamanyemaYerusalemuMapenziMatendo ya MitumeMkoa wa MaraUgonjwa wa kuharaNomino za kawaidaMungu ibariki AfrikaMazishiWilaya za Tanzania 4 KIGOMABarabaraBinamuTiba asilia ya homoniNadhiriRaisMamelodi Sundowns F.C.BibliaOrodha ya majimbo ya Marekani🡆 More