Uvumba

Uvumba (pia: ubani) ni utomvu mkavu (uliokauka) wenye harufu ya kupendeza ukichomwa.

Unapatikana kutoka miti ya aina Boswellia thurifera (pia: Boswellia sacra).

Uvumba
Gramu 100 za utomvu mkavu wa uvumba.
Uvumba
Uvumba kutoka Yemen.

Matumizi ya kidini

Matumizi yake ni katika ibada za kidini lakini pia nyumbani.

Mataifa ya kale ya Mashariki ya Kati yalitumia uvumba mahekaluni kwa mfano Wamisri, Wayahudi na Waroma wa Kale.

Kutoka kawaida ya Uyahudi, lakini pia ya Dola la Roma, matumizi yake yameingia katika Ukristo na katika liturujia za Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi.

Waprotestanti huwa hawaitumii isipokuwa sehemu za Waanglikana na Walutheri wenye mwelekeo wa kukazia urithi wa kiliturujia.

Matumizi ya kiganga

Kuna pia matumizi kama dawa ya kumeza kwa kusudi la kuimarisha akili na kumbukumbu lakini pia kwa kupambana na ugonjwa wa jongo.

Wamisri wa Kale waliitumia kwa kutunza maiti ya marehemu.

Biashara ya uvumba

Miti ya Boswellia hustawi katika maeneo yabisi kama Yemen, Omani, Somalia, Ethiopia na sehemu za Bara Hindi mbali na nchi zenye rutuba nzuri na watu wengi. Hivyo uvumba ulitafutwa sana na kufanyiwa biashara kama bidhaa ya thamani.

Katika taarifa za Injili ya Mathayo (kitabu cha Biblia ya Kikristo) uvumba ulikuwa kati ya zawadi zilizoletwa na mamajusi wa mashariki huko Bethlehemu kama zawadi kwa mfalme wa Wayahudi aliyezaliwa.

Tags:

MitiUtomvu

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

LahajaWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiVivumishi vya idadiKilimanjaro (Volkeno)LongitudoFasihi andishiKiwakilishi nafsiOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaMnara wa BabeliNyweleNdoa katika UislamuHistoria ya MongoliaAthari za muda mrefu za pombeUkoloniWema SepetuMisemoFIFAWapareFutiMaudhuiTupac ShakurKifaduroOrodha ya vitabu vya BibliaUmoja wa MataifaUfugaji wa kukuMajira ya baridiKontuaUmoja wa AfrikaPasakaWaluguruSean CombsJimbo Kuu la Dar-es-SalaamPasifikiOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaSaddam HusseinAngkor WatNamba tasaUandishi wa inshaHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoMarijani RajabMkoa wa ManyaraMtemi MiramboAli Hassan MwinyiMahindiManeno sabaMofolojiaFamiliaTamthiliaHoma ya iniKalenda ya KiislamuNguzo tano za UislamuSimba S.C.Tamathali za semiWiki FoundationKalendaMjusi-kafiriMahakama ya TanzaniaOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaJiografia ya UrusiUgonjwa wa kupoozaOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoWangoniKamusi ya Kiswahili sanifuHifadhi ya mazingiraAina za manenoUtumwaSanaaJuxMjombaHafidh AmeirJapaniAmri KumiLady Jay DeeViunganishiBahari ya HindiMkoa wa Tanga🡆 More