Udadisi (kwa Kiingereza: curiosity, kutoka neno la Kilatini curiositas, yaani umakini) ni tabia ya kuchunguza kitu au jambo kwa kina.
Mara nyingi wanasayansi ndio wadadisi wazuri kwa maana wao huchunguza kwa kina na umakini, wakifuata kanuni na kutafuta ushahidi. Kwa njia yao udadisi umestawisha maisha ya binadamu.
Katika udadisi kuna ule wa kawaida na mwingine usio wa kawaida. Kwa udadisi wa kawaida mtu hudadisi kwa njia rahisi, tofauti na ule usio wa kawaida ambapo mtu asipokuwa makini anaweza hata kufa. Udadisi huu unahitaji kuwa makini sana.
Udadisi unajitokeza mapema katika mtoto, lakini unapozidi na kuelekea mambo yasiyo na maana (kwa mfano umbeya) unamzuia mtu asijue mambo ya maana; hapo ni kilema cha akili.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Udadisi, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.