Theofredi Wa Thebe

Theofredi wa Thebe (pia: Chiaffredo, Chiaffredus, Theofredus, Ciafrè, Chaffre, Teofredo, Jafredo, Jafredus, Eufredus, Jofredus, Sinfredus, Zaffredus; alikuwa askari wa jeshi la Roma ya Kale katika kikosi cha Thebe kilichoongozwa na Morisi Mtakatifu.

Theofredi Wa Thebe
Mchoro mdogo wa Wat. Morisi na Theofredi.

Kufuatana na mapokeo ya karne ya 4 kikosi hicho kilijumlisha wanajeshi Waafrika kutoka Misri ya kusini na Nubia waliotumwa Ulaya wakati wa Kaisari Maximiano wa Roma. Wengi wao walikuwa Wakristo. Katika mapokeo ya sanaa ya Kikristo walichorwa kama Waafrika weusi.

Huko Agaunum (leo Saint-Maurice-en-Valais), karibu na mto Rhone, katika eneo la Uswisi wa leo, walipewa amri ya kujiandaa kwa mapigano dhidi ya waasi na kabla ya mapigano kutoa sadaka kwa Kaisari aliyeheshimiwa kama mungu mmojawapo. Wakristo hao walikataa kutoa sadaka hiyo. Kaisari alipopata habari hii akakasirika akatoa amri kuua kila askari wa kumi katika kikosi. Wakristo walipoendelea kukataa amri ilirudiwa hatimaye karibu kikosi chote kiliuawa pamoja na kiongozi chake Morisi.

Inasemekana Theofredi alifaulu kukimbia akafia dini huko Crissolo (Piemonte, Italia) .

Morisi pamoja na kikosi chake waliheshimiwa mapema kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu ya Theofredi huadhimishwa tarehe 7 Septemba.

Tazama pia

Tanbihi

Theofredi Wa Thebe  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.

Tags:

AskariJeshiKikosi cha ThebeMorisi MtakatifuRoma ya Kale

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Mbwana SamattaHifadhi ya Mlima KilimanjaroViwakilishi vya idadiKaswendeMuhammadMaskiniIsraelAli KibaKata za Mkoa wa Dar es SalaamMethaliGhanaUchaguzi Mkuu wa Tanzania, 2020Joseph ButikuDubaiUfugaji wa kukuInshaKinjikitile NgwaleLa LigaNadhariaOrodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watuYesuMfumo wa upumuajiNabii IsayaKinyongaMwakaTungoBahashaMkoa wa Dar es SalaamTenziMkoa wa SongweHifadhi ya Taifa ya NyerereDaktariBahari ya HindiCristiano RonaldoNembo ya TanzaniaFisiViwakilishi vya sifaMadiniVivumishiNyimbo za jadiUraibuWahaUkimwiMgonjwaNyotaHakiUsafi wa mazingiraUkatili wa kijinsiaJakaya KikweteMlo kamiliViwakilishi vya kumilikiUnyevuangaAmfibiaUandishi wa ripotiNg'ombeLisheSisimiziJoseph Sinde WariobaIdi AminWazaramoNgonjeraNguvaMshale (kundinyota)Mkoa wa DodomaMuungano wa Madola ya AfrikaDhahabuAzimio la Kimataifa juu ya Haki za BinadamuShuleBloguMaambukizi ya njia za mkojo🡆 More