Prometheus

Prometheus alikuwa mmoja wa miungu wa nasaba ya Watitani katika mitholojia ya Kigiriki.

Alitazamwa kuwa mwana wa Iapetos na Clymene, hivyo alikuwa mjukuu wa Uranos. Kati ya miungu mbalimbali ndiye Prometheus aliyeumba binadamu.

Prometheus
Prometheus akiteswa na tai, uchoraji kenye bakuli la divai la Ugiriki ya Kale.
Prometheus
Prometheus akiwa amefungwa mnyororo, taswira ya Peter Paul Rubens, 1611-1612.

Katika masimulizi ya Wagiriki wa Kale siku moja alimdanganya mungu mkuu Zeu; wakati wa sadaka alificha nyama nzuri iliyotakiwa kuchomwa na badala yake alitoa sehemu zisizokuwa na thamani, maana alitaka kuhifadhi nyama nzuri kwa ajili ya binadamu aliowahi kuumba. Hapo Zeu alikasirika, hivyo alikataa binadamu wasipate siri ya kutumia moto. Lakini Prometheo aliamua kuiba moto mbinguni na kuwaletea binadamu.

Zeu alikasirika akaamuru Prometheus afungwe kwa mnyororo kwenye milima ya Kaukazi. Kila siku alikuja tai aliyekula ini lake, ila wakati wa usiku ini lilikua upya, ili liliwe na tai siku iliyofuata. Prometheus alipaswa kuvumilia mateso haya miaka mingi hadi siku moja akaja shujaa Herakles aliyemwua tai na kumrudishia uhuru wake. Hatimaye Zeu alimsamehe akarudi katika baraza la miungu kwenye mlima Olimpos.

Masimulizi ya Prometheus yalipokewa na Waroma wa Kale ambako Prometheus alitazamwa mara nyingi kama mwalimu wa ubinadamu aliyekuwa chanzo cha elimu na sanaa. Baadaye hadithi zake zilijadiliwa katika sanaa, fasihi na falsafa ya Ulaya, hasa tangu zama za Mwangaza. Wengine walimchukua kama mfano wa maendeleo ya sayansi na teknolojia yanayomwezesha binadamu kutawala mazingira asilia. Wengine tena walimchukua kama mfano wa kiburi cha binadamu katika kutafuta maendeleo kwa kila njia, bila kutaka kukubali hali yake kama kiumbe, hivi kwamba anaharibu mazingira na maisha kwa jumla.

Tovuti nyingine

Tags:

BinadamuMitholojia ya KigirikiMiunguMjukuuMwanaUranoWatitanien:Asia (mythology)

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

KihusishiKishazi tegemeziMwanaumeMapenziJulian AssangeTreniViunganishiMnara wa BabeliOrodha ya kampuni za TanzaniaMunguMbuMagadi (kemikali)NevaKwaresimaBurundiRwandaKifaduroNdiziNgome ya YesuVitenzi vishiriki vipungufuFananiMpira wa kikapuBenjamin MkapaJanuary MakambaKinyongaImaniUmaskiniBruneiNabii EliyaUmoja wa KisovyetiBob MarleyShetaniKitenziInsha za hojaMtemi MiramboMkoa wa SongweMkoa wa DodomaUgonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofunganaAmfetaminiRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniRihannaJipuRisalaKiini cha atomuHali ya hewaWikiSaratani ya mapafuTungo kiraiOrodha ya vitabu vya BibliaMichezoUtamaduniVivumishi vya pekeeDjigui DiarraAbedi Amani KarumeNyaniRiadhaVichekeshoKitabu cha ZaburiStadi za lughaIsraeli ya KaleSanaaMichezo ya jukwaaniKuhaniTaasisi ya Taaluma za KiswahiliKifo cha YesuMaudhuiMweziLughaUmoja wa Muungano wa AfrikaHifadhi ya NgorongoroKuhani mkuuMamba (mnyama)NyongoNdoaFamilia🡆 More