Pluto

Kuhusu matumizi ya jina Utaridi kwa sayari hii tazama chini kwa jina

134340 Pluto
Pluto, New Horizons mnamo Julai 2015.
Pluto, New Horizons mnamo Julai 2015.
Ugunduzi
MgunduziClyde W. Tombaugh
Tarehe18 Februari 1930
Jina
Asili ya jinaKla. Plūtō, kutokana na Kgk. Πλούτων (Ploutōn)
AlamaPluto na Pluto
Tabia za njiamzingo
Umbali mfupikm 4,436,820,000
au 29.658
Umbali mrefukm 7,375,930,000
au 49.305
km 5,906,380,000
au 39.482
Uduaradufu0.2488
siku 90,560
miaka 247.94
Mwinamo17.16°
Miezi5
Tabia za kimaumbile
km 1,188.3±0.8
mara 0.1868 ya Dunia
mara 0.684 ya Mwezi
Tungamokg (1.303±0.003)×1022
mara 0.00218 ya Dunia
mara 0.177 ya Mwezi
g/cm3 1.854
Uvutano wa usoni
m/s2 0.620
Kasi ya kuponyokea
km/s 21.3
siku −6.38680
siku −6.387230
Weupe0.72 (Bond)
0.52 (jiometri)
HalijotoK 44 (−229°C)
Pluto
Njia ya Pluto ya kuzunguka jua inakata njia ya Neptune - hali halisi njia ya Pluto ni duaradufu

Pluto (alama: ⯓ au ♇) ni sayari kibete inayozunguka jua ng'ambo ya obiti ya Neptuni.

Masi yake ni hasa mwamba na barafu. Kipenyo chake ni km 2,390.

Katika mwendo wake inakata njia ya Neptune kwa sababu njia yake ina umbo la duaradufu kali.

Miezi

Pluto ina miezi mitano inayoitwa Charon, Styx, Nix, Kerberos na Hydra. Charon ni kama nusu ya ukubwa wa Pluto (kipenyo km 1200) na umbali wa wastani ni km 19,410. Styx, Nix, Kerberos na Hydra ni miezi midogo (vipenyo: km 10-25, 56x26, 31 na 43x33) yenye umbali wa km 42,600, 48,600, 57,700 na 64,700 kutoka Pluto.

Sayari au sayari kibete?

Pluto ilikuwa ikitambulika kama sayari ya tisa katika mfumo wa Jua toka mwaka 1930 hadi Agosti 2006. Vipimo vipya vilileta wasiwasi juu ya swali: Je, sayari ni kitu gani?, hasa baada ya kugundua magimba ya ziada nje ya Pluto yanayokaribia ukubwa wake lakini hayafai kuitwa sayari.

Umoja wa kimataifa wa wanaastronomia uliondoa Pluto katika orodha ya sayari kwenye mkutano wake wa mwaka wa 2006. Badala yake wameiita sayari kibete. Hata hivyo baadhi ya wanaastronomia walipinga uamuzi huu.

Jina

Jina "Pluto" linamtaja mungu mtawala wa kuzimu katika mitholojia ya Roma ya Kale. Limechaguliwa kwa sayari hii kutokana na umbali wake na jua na giza kubwa liliko sawa na hali ya giza ambayo ni mfano wa kuzimu.

Vitabu kadhaa vinatumia jina la Kiswahili Utaridi kwa kufuata kamusi ya KAST; lakini mabaharia Waswahili wametumia jina hili la "Utaridi" tangu miaka mingi kwa ajili ya sayari ya kwanza (ing. "Mercury").

Marejeo

Viungo vya nje

Pluto 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
Pluto  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pluto kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Pluto MieziPluto Sayari au sayari kibete?Pluto JinaPluto MarejeoPluto Viungo vya njePluto

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Arusha (mji)Kitenzi kishirikishiVihisishiMiikka MwambaNdoaYatimaUbongoWapareSanaaMtandao wa kompyutaHuduma ya kwanzaRafikiBibi Titi MohammedNafsiVidonge vya majiraDuniaLughaAsiaUtakatifuDagaaManchester United F.C.LugarawaHistoria ya WapareUtoaji mimbaHussein KaziNyati wa AfrikaPemba (kisiwa)Nomino za kawaidaUgonjwa wa kuharaSteven KanumbaVielezi vya mahaliKenyaChawaDhanaMohamed HusseiniMkoa wa PwaniUingerezaNdotoLatitudoRwandaAfrika Mashariki 1800-1845Uundaji wa manenoOrodha ya hospitali nchini TanzaniaKiunguliaTanzaniaVita Kuu ya Pili ya DuniaUfugaji wa kukuKlamidiaHekalu la YerusalemuMeno ya plastikiMsituKanisa la Kiinjili la Kilutheri TanzaniaDubai (mji)Ihefu F.C.Eneo la utawalaPentekosteUmaskiniOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaMzabibuMaradhi ya zinaaMwanaumeKitabu cha YoshuaMsalaba wa YesuIdhaa ya Kiswahili ya Radio TehranKiraiNomino za wingiSamariaWasukumaNamba ya mnyamaNchiMweziLugha za KibantuMillard Ayo🡆 More