Pamba

Kwa matumizi mbalimbali ya neno hili angalia hapa

Pamba ni nyuzi nyeupe na laini zinazotokana na tunda la mpamba (Gossypium sp.). Nyuzi hizi zinaonekana kama sufi na mipamba inalimwa kwa nyuzi hizi ambazo ni msingi wa kutengeneza kitambaa na nguo.

Pamba
Pamba tayari kwa mavuno

Ndani ya tunda nyuzi za pamba zinaunganishwa na punje za mbegu wa mmea. Kusudi yao ni kusambaza mbegu kwa sababu zinafanya kazi kama tanga zinashika nguvu ya upepo na kuwezesha mbegu kuelea hewani mbali kiasi.

Pamba yenyewe inapatikana kutoka spihi nyingi za gossypium zinazokua kiasili katika sehemu mbalimbali za dunia. Lakini karibu pamba yote inayolimwa kwa matumizi ya nguo imetokana na spishi nne za mipamba ambazo ni

  • Gossypium herbaceum L. (asili ya Asia)
  • Gossypium arboreum L. (asili ya Asia)
  • Gossypium hirsutum L. (asili ya Amerika)
  • Gossypium barbadense L. (asili ya Amerika).

Kitambaa cha pamba huwa na faida nyingi kuliko vitambaa vya sintetiki. Pamba inaweza kushika unyevu hadi asilimia 80% ya uzito wake hivyo kitambaa chake kinapendeza hasa katika mazingira ya joto kwa sababu mtu husumbuliwi sana na jasho.

Pamba
Mipamba shambani
Pamba
Fukusitunda (Anthonomus grandis) anakula mpamba na kutaga mayai ndani ya matunda yake na kuharibu mavuno
Pamba
Mavuno ya kisasa kwa kutumia mashine inayovuna pamba na kuigandamiza kama mabloku makubwa kwa usafiri

Mavuno duniani 2004/2005

2004/2005 jumla ya tani 26.043.000 t za pamba zilivunwa duniani. Nchi zenye mavuno kubwa zilikuwa zifuatazo:

Nchi zenye mavuno makubwa ya pamba (2004/05)
 Rang  Nchi Mavuno (kwa t elfu) Asilimia ya mavuno ya dunia
   1 China    6.320 24,27 %
   2 USA    5.062 19,44 %
   3 Uhindi    4.080 15,67 %
   4 Pakistan    2.415 9,27 %
   5 Brasilia    1.250 4,80 %
   6 Usbekistan    1.134 4,36 %
   7 Afrika ya Magharibi1    1.040 3,99 %
   8 Uturuki    900 3,46 %
   9 Australia    613 2,35 %
   10 Ugiriki    390 1,50 %
   11 Syria    331 1,27 %
   12 Misri    291 1,12 %
   13 Turkmenistan    203 0,78 %
   14 Tajikistan    172 0,66 %
   15 Kazakhstan    148 0,57 %
    Wengine    1.694 6,51 %
    Dunia yote    26.043 100,00 %
(1) Afrika ya Magharibi inajumlisha Benin (152), Burkina Faso (257), Kamerun (105), Chad (85), Cote d'Ivoire (130), Mali (240) na Togo (71)
Pamba  Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pamba kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Uenezi wa KiswahiliNg'ombeWapareInshaNdovuSarufiJipuMartha MwaipajaHali ya hewaViwakilishi vya kumilikiYesuBarack ObamaMkoa wa TaboraAbedi Amani KarumeNdoto ya AmerikaMaambukizi nyemeleziUtamaduni wa KitanzaniaEthiopiaHistoria ya ZanzibarOrodha ya kampuni za TanzaniaLigi Kuu Uingereza (EPL)CherehaniJogooHistoria ya KanisaFonetikiVitenzi vishiriki vipungufuNabii IsayaYouTubeWasukumaJokofuBorussia DortmundTwigaVidonda vya tumboDhanaNyasa (ziwa)KiunguliaHistoria ya WokovuTarafaUnyevuangaMkoa wa ManyaraMtaalaDodoma (mji)Orodha ya Marais wa MarekaniNathariOrodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watuInsha za hojaVielezi vya idadiHadubiniFananiMnazi (mti)Kitenzi kishirikishiMachweoHoma ya matumboKomaMwanza (mji)Mwanzo (Biblia)SumakuNigeriaTungo kiraiUshairiNandyUkwapi na utaoMaana ya maishaMkoa wa KigomaWahangazaRitifaaMtiMkoa wa MorogoroUpendoDawatiLugha za KibantuBurundiKiburi🡆 More