Ndimu

Ndimu ni tunda la mndimu (Citrus aurantiifolia), mti wa familia ya michungwa (Rutaceae).

Ndimu
Ndimu mbichi mtini.

Umbo lake ni mduara wenye rangi ya kijani mpaka njano, na kipenyo cha sm 3-6.

Lina ladha ya uchachu kwa sababu ya asidi ndani yake. Ndimu mara nyingi hutumika kuongeza ladha kwenye chakula na vinywaji. Kwa kawaida ni dogo kuliko limau, na chanzo kizuri pia cha vitamini C.

Katika kanda za tropiki na nusutropiki mindimu inaweza kumea mwaka wote maji yakiwapo. Ndimu huweza kuwa chungu au tamu. Ndimu chungu huwa na kiasi kikubwa cha sukari na asili ya asidi citric kuliko malimao na kuwa na ladha ya asili huku ndimu tamu hukosa asidi ndani yake hivyo kuwa na ladha tamu kwelikweli.

Ndimu ni matunda madogo, ambayo ngozi na nyama yake ni kati ya inchi moja au mbili hivi.

Matumizi

Kupikia

Ndimu 
Tunda bivu lililokatwa
Ndimu 

Katika mapishi ndimu huthaminiwa kwa yote, ladha yake ya asidi na harufu yake ya kukoza ni viungo maalumu sana kwa vyakula vya Meksiko, Vietnamu, Thailandi na kusini mashariki mwa Marekani. Zaidi hata majani ya mmea wa ndimu hutumika kwenye mapishi, hasa katika nchi za Asia. Majani ya mmea huo hutumika kama dawa pia katika maeneo mengi, hasa kusini na mashariki mwa Asia .

Virutubisho kwa gramu 100 (3.5 oz) Nishati 126 kJ (30 kcal) Kabohaidreti11 g Sukari1.7 g Makapi3 g Mafuta0.2 g Protini0.7 g Maji88 g Vitamini C29 mg (48%)

Matumizi mengine

Katika kutibu ugonjwa wa ngozi, kiseyeye mnamo karne ya 19, serikali ya Uingereza ilihimiza watu wale sana ndimu, hii ni kutokana na kuwa chanzo kizuri cha vitamini C.

Pamoja na mafuta maalumu, maji ya limao pia hutoa mchanganyiko unaotumika katika matengenezo ya marashi. Baadhi ya watu hunyunyiza maji ya ndimu kwenye macho yao, kupata uoni mzuri. Huko India hutumika kufukuza roho wabaya.

Uzalishaji

India inaongoza kwa kuzalisha malimao na ndimu kwa wingi zaidi kwa asilimia 16, ikifuatwa na Meksiko (14. 55%), Ajentina (10%), Brazili (85%) na Hispania (7%)

Tags:

Ndimu MatumiziNdimu UzalishajiNdimuCitrus aurantiifoliaFamilia (biolojia)MichungwaMndimuMtiTunda

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

NahodhaPasaka ya KikristoAzimio la ArushaLeonard MbotelaTaasisi ya Taaluma za KiswahiliKupatwa kwa MweziOrodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watuOrodha ya Watakatifu WakristoHistoria ya IsraelJogooAdolf HitlerJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaKundiMbogaTausiMunguUsalamaRwandaMwigizajiDhima ya fasihi katika maishaAdhuhuriYesuMkoa wa DodomaNevaAli Hassan MwinyiMakaburuDawa za mfadhaikoUsafi wa mazingiraHistoria ya KanisaHadhiraUsultani wa ZanzibarNileTambaziSayariHurafaJinaiKamusiLenziJiniMtakatifu PauloTabainiWallah bin WallahVolkenoNyweleFisiKata za Mkoa wa Dar es SalaamKaziNgano (hadithi)MamaStephane Aziz KiTanganyika (ziwa)MaktabaAlama ya uakifishajiLugha za KibantuUtohoziVivumishi vya idadiMwaka wa KanisaOrodha ya nchi za Afrika kulingana na pato la taifaMkoa wa LindiMaskiniSamakiUtamaduniMaudhuiNyotaMoses KulolaInshaMiundombinuUturukiHistoria ya TanzaniaWilaya ya HandeniHifadhi ya mazingiraWaluguruJumuiya ya Madola🡆 More