Mzee Simeoni alikuwa mwanamume mwadilifu wa Yerusalemu (leo nchini Palestina/Israeli) katika karne ya 1 KK.
Ni maarufu hasa kwa kumpakata mtoto Yesu alipoletwa na wazee wake katika hekalu la Yerusalemu siku 40 tu baada ya kuzaliwa Bethlehemu.
Kadiri ya Injili ya Luka (2:25-35) alikwenda kumlaki kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu aliyekuwa amemuahidia hatakufa kabla hajamuona Masiya.
Alipomtambua katika mtoto huyo alishangilia na kumsifu Mungu kwa wimbo maarufu alipomtangaza Yesu kuwa ndiye wokovu ulioandaliwa kwa mataifa yote.
Baada ya hapo alimtabiria Bikira Maria kwamba upanga utamchoma moyo kuhusiana na upinzani utakaompata mwanae.
Tangu kale anaheshimiwa na madhehebu mengi ya Ukristo kama mtakatifu, hasa tarehe 2, 3 au 15 Februari.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mzee Simeoni kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mzee Simeoni, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.