Mikrobiolojia

Mikrobiolojia (kutoka maneno ya Kigirikiμῑκρος, mīkros, ndogo; βίος, bios, uhai; na λογία, logia, elimu) ni fani inayochunguza vidubini vyenye seli moja, nyingi au visivyo nayo kabisa.

Mikrobiolojia ina matawi yake, yakiwemo virolojia, mukolojia, parasitolojia na bakteriolojia.

Mikrobiolojia
Agar plate iliyojaa vidubini.
Mikrobiolojia
Antonie van Leeuwenhoek, mwanamikrobiolojia wa kwanza na mtu wa kwanza aliyeona bakteria kwa darubini.

Bakteria ziligunduliwa mara ya kwanza na Antonie van Leeuwenhoek mwaka wa 1676, kwa kutumia darubini ya lensi moja ya muundo wake mwenyewe. Aliziita "animalcules" na alichapisha habari za utafiti wake kwenye msururu wa barua kwa Shirika la Muungano wa Mfalme. Jina bacteriam lililetwa miaka mingi baadaye, na Christian Gottfried Ehrenberg katika mwaka wa 1838.

Mwaka 1859 Louis Pasteur alionyesha kuwa mchakato wa kuchachusha unasababishwa na ukuaji wa vijiumbe, na kwamba ukuaji huu si wa kizazi cha kujianzia. (Hamira na kuvu, ambazo kwa kawaida zinahusishwa na uchachushaji, si bakteria, ila ukungu.) Pamoja na mwenzake, Robert Koch, Pasteur alikuwa wa kwanza kuitetea nadharia ya kijidudu ya ugonjwa.

Robert Koch alikuwa mwanzilishi wa taaluma ya uuguzi wa mikrobiolojia na alishughulikia kipindupindu, kimeta na kifua kikuu. Katika utafiti wake wa kifua kikuu, Koch hatimaye alithibitisha nadharia ya kijidudu, ambayo ilimfanya atunukiwe Tuzo la Nobel mwaka wa 1905. Katika madai yake, Koch aliweka vigezo vya kutathmini kama kiumbe ndicho husababisha ugonjwa, na madai haya yanatumika mpaka leo hii.

Ingawa katika karne ya 19 ilijulikana kwamba bakteria ndizo chanzo cha magonjwa mengi, hakuna matibabu yoyote ya viua-bakteria yaliyopatikana. Katika mwaka wa 1910, Paul Ehrlich alitengeneza kiua vijasumu cha kwanza, kwa kubadilisha rangi ambazo kwa kuchagua zilitia mawaa Treponema pallidum, spirokaeti ambayo husababisha kaswende katika mchanganyiko wa ambao uliua kisababishi magonjwa. Ehrlich alikuwa ametuzwa Tuzo la Nobel mwaka 1908 kwa kazi yake kuhusu elimu ya kingamaradhi, na alianzisha matumizi ya madoa ili kuchunguza na kubaini bakteria, na kazi yake ilijikita kwenye misingi ya doa la Gram na doa la Ziehl-Neelsen.

Mafanikio makubwa katika utafiti wa bakteria yalikuwa kutambuliwa kwa Carl Woese mwaka 1977 kwamba akea zilishuka kutokana na mabadiliko tofauti kutoka yale ya bakteria. Uanishaji huu mpya wa jamii ya filojenetiki ulikitwa kwenye misingi ya kufululizwa kwa ribosomu RNA 16S, na ukagawa prokaryota katika makundi mawili yenye mageuko tofauti, kama mojawapo ya sehemu ya mifumo ya vikoa vitatu.

Tanbihi

Viungo vya nje

Mikrobiolojia 
Wiki Commons ina media kuhusu:
Mikrobiolojia  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mikrobiolojia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

BakteriolojiaKigirikiNenoSeliUhaiVidubini

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

KitenziJeff BezosNathariLucky DubeWapareHarmonizeNgonjeraIsraeli (maana)Kifo cha YesuMkunduManchester CityKanisa la Anglikana la TanzaniaUsafi wa mazingiraHistoriaMkoa wa KilimanjaroAkiliBayer 04 LeverkusenWaanglikanaFananiSakramentiAfyaJumuia ndogondogo za KikristoKupatwa kwa MweziHadubiniMofolojiaOrodha ya makabila ya TanzaniaShetaniShambaUaminifuMaambukizi ya njia za mkojoMuhammadHistoria ya KanisaKipepeoMisale ya waaminiTabiaKifua kikuuMkoa wa GeitaEdward Ngoyai LowassaMungu ibariki AfrikaRaiaWamanyemaEkaristiMwanzo (Biblia)Mohamed HusseiniOrodha ya milima ya mkoa wa MbeyaAmri KumiAfrikaMitaNyaraka za PauloMapinduziVihisishiMkurugenziBikiraMsamahaKarafuuMfumo wa JuaMuundo wa inshaSanaaNabii EliyaMuungano wa Tanganyika na ZanzibarMshubiriRwandaBiasharaMishipa ya damuSamia Suluhu HassanYordaniUzazi wa mpangoJinsiaKirenoOrodha ya Watakatifu wa Afrika🡆 More