Mankala ni jina la kimataifa kwa michezo inayofanana na bao.
Ni kundi la michezo kwa wachezaji wawili wanaohamisha kete (vijiwe, mbegu) kati ya nafasi zilizopangwa, mara nyingi mashimo katika bodi ya bao, ardhini au katika jiwe.
Michezo ya mankala inachezwa mahali pengi duniani. Inapendwa sana Afrika na Asia. Michezo hizi, zilitoka Africa.
Kwa kawaida, watu wawili wanacheza. Wanaweka kete ndani ya shimo. Mchezaji mmoja anachagua shimo, anatoa kete, na anaziweka kwa shimo zingine moja kwa moja. Wachezaji wanajaribu kupata kete nyingi zaidi ili washinde. Lakina, kuna aina nyingi na kanuni tofauti za kukamata kete na kuziweka kwa shimo. Pia, michezo hizi za aina ya mankala zina idadi ya shimo tofauti. Lakini michezo hii yote ni michezo ya akili, na inasomesha watu kufanya hesabu. Kwa hivyo, watu wanapenda kuwafundisha watoto wao kucheza.
Jina la Mankala linatumikakwa aina ya michezo tofauti, na kwa familia ya michezo. Jina hili ni la Kiarabu (منقلة), na linafanana na naqala (نقلة), yaani kuendelea.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Mankala, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.