Kuhara

Kuhara au kuendesha ni hali ya kupata choo chepesi au cha majimaji angalau mara tatu kwa siku. Kwa kawaida hudumu kwa siku chache na inaweza kusababisha upungufu wa maji mwilini kwa sababu ya ukosefu wa maji. Ishara za upungufu wa maji mwilini kwa kawaida huanza na ukosefu wa kunyooka kwa kawaida kwa ngozi na mabadiliko katika tabia za mtu. Hii inaweza kuendelea na kusababisha upungufu wa mkojo, upungufu wa rangi ya ngozi, a mpigo wa haraka wa moyo, na upungufu wa mwitikio inapoendelea kuwa mbaya zaidi. Hata hivyo, huenda kinyesi chepesi lakini kisicho cha majimaji katika watoto wanaonyonya, kikawa cha kawaida.

Kuhara
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyInfectious diseases, Gastro-enterolojia Edit this on Wikidata
ICD-10A09., K59.1
ICD-9787.91
DiseasesDB3742
MedlinePlus003126
eMedicineped/583
MeSHD003967

Sababu kuu ya maambukizo ya matumbo huwa ni kwa sababu ya kvirusibakteriakimelea, au hali inayojulikana kama gastroenteritis. Maambukizo haya kwa kawaida hupatikana kutokana na chakula au maji ambayo yameambukizwa na kinyesi, au moja kwa moja kutoka kwa mtu mwingine ambaye ameambukizwa. Huenda ikagawanywa kwa aina tatu: kuhara maji kwa muda mfupi, kuhara damu kwa muda mfupi, na ukiwa utadumu kwa zaidi ya wiki mbili, kuhara kunaoendelea. Kuhara maji kwa muda mfupi huenda kukasababishwa na maambukizo ya kipindupindu. Ikiwa kuna damu inajulikana kama kuhara. Kuna sababu kadhaa zisizo za kuambukizwa ambazo zinaweza pia kusababisha kuhara ikiwa ni pamoja na: hyperthyroidism, kutovumilia laktosi, ugonjwa wa kuvimba matumbo, baadhi ya dawa, na ugonjwa wa matumbo yanayowashwakati ya sababu nyingine. Katika visa vingi uchunguzi wa kinyesi hauhitajiki ili kuthibitisha sababu halisi.

Unaweza kuzuia kuhara kunaoweza kuambukizwa kwa usafi ulioboreshwa, maji masafi ya kunywa, na kunawa mikono. Kunyonyesha kwa angalau miezi sita kunapendekezwa hata pia chanjo dhidi ya rotavirus. Dawa ya maji ya kunywa (ORS), ambayo ni maji masafi yenye viwango vinavyofaa vya chumvi na sukari, ndio matitabu yanayopendekezwa. Tembe za Zinki zinapendekezwa pia. Matibabu haya yamekadiriwa kuwa yamewaokoa watoto milioni 50 kati ya miaka 25 iliyopita. Wakati watu wanahara inapendekezwa kwamba waendelee kula chakula chenye afya na watoto waendelee kunyonya. Ikiwa ORS ya kuuzwa hazipatikani, suluhisho za nyumbani zinaweza kutumiwa. Kwa wale wanoendesha sana, maji ya kudungwa ndani ya venayanaweza kuhitajika. Hata hivyo, katika visa vingi, inaweza kudhibitiwa vizuri kwa maji mdomoni. Viua wadudu, ijapokuwa haitumiwi sana, inaweza kupendekezwa katika visa vichache kama wale wanaohara damu na wana joto jingi, kuhara kunaotokana na kusafiri, na wale wanaopata bakteria au vimelea fulani katika kinyesi chao. Loperamide inaweza kusaidia kupunguza kuhara lakini haipendekezwi kwa wale wenye maradhi makali.

Karibu visa bilioni 1.7 hadi 5 za kuhara hufanyika kila mwaka. Vimekita mizizi sana katika nchi zinazokua, ambapo watoto wadogo wanahara karibu mara tatu kwa mwaka. Duniani kote, hadi 2012, ilikuwa sababu ya pili kuu ya watoto kufariki wakiwa chini ya miaka 5 (milioni 0.76 au 11%). Matukio ya mara kwa mara ya kuhara huwa sababu kuu ya utapiamlo na sababu kuu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano. Matatizo mengine ya muda mrefu ambayo yanaweza kutokea ni pamoja na ukuaji duni wa kimwili na kiakili.

Marejeleo

Tags:

Mkojo

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

WajitaNdovuTaarabOrodha ya milima ya TanzaniaFacebookWokovuUtandawaziNdege (mnyama)SamariaDayolojiaWapareLilithBonde la Ufa la Afrika ya MasharikiAina za udongoMchwaMkoa wa Unguja Mjini MagharibiBungeMizimuMichael JacksonMariooNenoUbongoUkimwiJapaniPichaNomino za pekeeYohane MbatizajiOrodha ya visiwa vya TanzaniaEe Mungu Nguvu YetuIsimujamiiSanduku la postaUzazi wa mpango kwa njia asiliaKukiUtataItifakiSaa za Afrika MasharikiNomino za kawaidaOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaCleopa David MsuyaKonrad LorenzMalariaLiverpool F.C.Orodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaShengNgw'anamalundiSimuUmmy Ally MwalimuUzazi wa mpangoMenoMartha MwaipajaDubuOrodha ya majimbo ya MarekaniBiasharaMsokoto wa watoto wachangaKiambishi awaliKanuni ya Imani ya MitumeMbuniChuiNgano (hadithi)JinaUwanja wa Taifa (Tanzania)Orodha ya Magavana wa TanganyikaMeta PlatformsOrodha ya makabila ya KenyaLuteni KanaliMamba (mnyama)Bustani ya EdeniMuundoMapacha (kundinyota)Jumuiya ya MadolaNandyOrodha ya Marais wa BurundiMlima MeruMtume BartolomayoWizara za Serikali ya TanzaniaWema Sepetu🡆 More