Kosta Rika

Kosta Rika (kwa Kihispania: Costa Rica, yaani Pwani Tajiri) ni nchi ya Amerika ya Kati.

Kosta Rika
Kosta Rika
Ramani ya Kosta Rika.

Imepakana na Nikaragua na Panama; kuna pwani ya Pasifiki upande wa magharibi na pwani ya Bahari ya Karibi upande wa mashariki.

Kosta Rika ilikuwa nchi ya kwanza duniani ya kufuta jeshi lake kikatiba. Pia inaongoza kwa kuhifadhi mazingira.

Mji mkuu ni San José.

Historia

Kabla ya kufika kwa Wahispania katika karne ya 16, nchi ilikaliwa na Waindio wachache.

Mwaka 1821 koloni hilo lilijiunga na ghasia ya maeneo mengine ya Amerika ya Kati dhidi ya utawala wa Hispania.

Mwanzoni nchi hizo ndogo zilijiunga na Meksiko lakini baada ya miaka miwili zilianzisha "Shirikisho la Amerika ya Kati" lililokwisha mwaka 1839.

Tangu mwaka 1847 Kosta Rika imekuwa nchi ya kujitegemea kabisa.

Mwaka 1948 kulitokea vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo viliwahi kwisha. Mwaka uliofuata nchi ilifuta kabisa jeshi hadi leo.

Watu

Wakazi wengi (65.8%) wana asili ya Ulaya, mbali ya machotara Wazungu-Waindio (13.65%) na wahamiaji wenye asili yoyote (9.03%). Waindio, ambao ndio wakazi asili, ni 2.4% tu.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kihispania.

Upande va dini, walio wengi ni wafuasi wa Yesu katika Kanisa Katoliki (70.5%: ndiyo dini rasmi) au madhehebu ya Uprotestanti (13.08%). Nje ya Ukristo, unaongoza Ubuddha (2.3%).

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Kosta Rika 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
Kosta Rika  Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika ya Kati bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kosta Rika kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Kosta Rika HistoriaKosta Rika WatuKosta Rika Tazama piaKosta Rika TanbihiKosta Rika Viungo vya njeKosta RikaAmerika ya KatiKihispania

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Maajabu ya duniaKipindupinduWayahudiBenki ya DuniaMzabibuVidonda vya tumboJinaUkoloniMwongoUaMofuOrodha ya milima mirefu dunianiTashihisiUandishi wa ripotiChakulaHaki za watotoMkondo wa umemeLigi ya Mabingwa AfrikaBendera ya KenyaKing'amuziKidoleMbogaAzimio la ArushaRitifaaNdimuRamaniUtataAsiaMpira wa mkonoPemba (kisiwa)MazungumzoMkoa wa ManyaraFonolojiaMsokoto wa watoto wachangaBarua pepeIsimilaHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoNdoa katika UislamuIsimujamiiHali ya hewaUhalifu wa kimtandaoPumuMwanzoKhadija KopaUjerumaniHedhiHistoria ya EthiopiaJumuiya ya MadolaMtakatifu MarkoRoho MtakatifuUdongoHeshimaMwenge wa UhuruSerikaliSumbawanga (mji)MbagalaMadhara ya kuvuta sigaraMichezo ya watotoKumaTanganyika (ziwa)Biashara ya masafa marefu ya Afrika MasharikiWikipediaMbuga za Taifa la TanzaniaKunguniAsili ya KiswahiliMweziKishazi huruKinyakyusaMatiniKataVivumishi vya urejeshiFasihiSemantikiKichecheMkoa wa Shinyanga🡆 More