Kisilesia (kwa Kisilesia: ślůnsko godka, ślůnski, pia huitwa pů našymu) ni lugha izungumzwayo na watu wa mkowa wa Upper Silesia nchini Poland, lakini pia kinazungumzwa katika nchi ya Ucheki na Ujerumani.
Mnamo mwaka wa 2011, imetangazwa kuwa takriban 509,000 Kisilesia kuwa kama lugha yao fasaha.
Kisilesia kina husiana kwa karibu sana na lugha ya Kipolandi, na ndiyomaana kinafikiriwa na wanasiimu wengi kuwa kina lafudhi ya Kipolandi.
Hakuna herufi moja tu ya Kisilesia. Wazungumzaji wa Kisilesia hutumia kuandika kilugha hiki kwa kufuata taratibu za uandikaji wa Kipolandi. Mnamo mwaka wa 2006 imegunduliwa herufi mpya za Kisilesia, ipo katika misingi ya Kisilesia tu (kuna misingi ipatayo 10). Kina tumika sana katika mtandao wa Internet, kama vile jinsi kinavyotumika katika Wikipedia ya Kisilesia.
Aa Bb Cc Ćć Čč Dd Ee Ff Gg Hh Ii Jj Kk Ll Mm Nn Ńń Oo Pp Rr Řř Ss Śś Šš Tt Uu Ůů Ww Yy Zz Źź Žž
Na baadhi ya herufi za ziada: Ch Dz Dź Dž.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Kisilesia, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.