Kikatalunya au kikatalani (kwa Kikatalunya: català) ni mojawapo kati ya lugha za Kirumi ambayo ni lugha rasmi ya jimbo la Katalunya, Valencia na visiwa vya Baleari katika ufalme wa Hispania (Ulaya kusini magharibi) na vilevile utemi wa Andorra.
Pia inatumika katika sehemu za Ufaransa kusini na Italia visiwani.
Wanaoitumia kama lugha ya kwanza ni watu milioni 4.1 na kama lugha ya pili ni milioni 5.1.
Asili ya lugha hiyo ni katika nchi ya Hispania, na lugha iliyoizaa ni Kilatini cha Waroma wa Kale waliotawala kwa muda mrefu Hispania.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kikatalunya kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Kikatalunya, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.