Wilaya

Wilaya ni mgawanyo wa kiutawala au eneo lililotengwa kwa ajili ya utawala.

Mikoa ya Tanzania na Kenya imegawiwa kwa wilaya.

Asili ya neno ni Kiarabu "ولاية" (wilaayatun - Kituruki: vilayet). Katika Dola la Osmani "vilayet" ilikuwa ngazi ya kwanza ya mgawanyo wa kiutawala ikimaanisha jimbo au mkoa. Mkuu wake au gavana alikuwa na cheo cha "Wali". Neno hili la "wilaya" limepatikana katika nchi nyingi zilizoathiriwa na utamaduni wa Uislamu au lugha ya Kiarabu kama vile Uturuki, Algeria, Tunisia, Oman, Mauritania, Sudan, Malaysia, Indonesia, Afghanistan, Tajikistan, Turkmenistan na Uzbekistan.

Katika Kiarabu cha Kisasa "wilaayatun" inamaanisha pia dola ndani ya shirikisho - kwa mfano madola kama vile Texas ndani ya Marekani.

Katika matumizi ya Kiswahili huko Kenya na Tanzania "wilaya" imekuwa mgawanyo wa ngazi ya pili yaani ni kitengo chini ya ngazi ya kwanza ya mikoa. Vitengo vya wilaya ni tarafa. Na vitengo vya tarafa ni kata zinazoitwa shehia katika Zanzibar na chini yake vijiji au mitaa.

Algeria ni nchi nyingine ambako wilaya inamaanisha ngazi ya pili ya kiutawala.

Tags:

KenyaMkoaTanzania

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Vita vya KageraMaajabu ya duniaNevaMobutu Sese SekoStadi za lughaUkimwiIdhaa ya Kiswahili ya Radio TehranKitomeoTiktokNyaniTambikoReal MadridJinsiaZama za ChumaUbongoHektariCleopa David MsuyaVielezi vya namnaFonimuSimuHoma ya matumboKunguniSayansiNgeliNguzo tano za UislamuManchester CityHorusNabii IsayaKamusi za KiswahiliOrodha ya maziwa ya TanzaniaKilwa KisiwaniPaul MakondaMatendo ya MitumeMajira ya mvuaFutiUwanja wa Taifa (Tanzania)SkeliViwakilishi vya kuulizaTendo la ndoaChawaKiimboAngahewaMaambukizi ya njia za mkojoMkoa wa Dar es SalaamKupatwa kwa MweziNdiziJoseph Sinde WariobaWanyamweziMbwana SamattaMaadiliYouTubeNzigeNetiboliNamba tasaMaambukizi nyemeleziSimu za mikononiNyangumiMimba kuharibikaWikipediaMbuniMuunganoMkoa wa MorogoroUenezi wa KiswahiliKinembe (anatomia)Mauaji ya kimbari ya RwandaNungununguHuzuniIsimuMkoa wa KageraClatous Chama22 ApriliBawasiriHifadhi ya SerengetiMjomba🡆 More