Isaac Asimov

Kigezo:Tfm

Isaac Asimov
Isaac Asimov
Bornmnamo 2 Januari 1920
Petrovichi, Smolensk Oblast, Urusi
Died 6 Aprili 1992
Brooklyn, New York City, Marekani
OccupationMwandishi, profesa wa biokemia
CitizenshipUrusi (utotoni), Marekani
Education
Alma materChuo Kikuu cha Columbia
GenresBunilizi ya kisayansi, mystery
Subjectssayansi, masimulizi,
Literary movementGolden Age of Science Fiction
Spouse(s)
  • Gertrude Blugerman (m. 1942–1973) «start: (1942)–end+1: (1974)»"Marriage: Gertrude Blugerman to Isaac Asimov" Location: (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Isaac_Asimov)
  • Janet Opal Jeppson
    (m. 1973–present) «start: (1973)»"Marriage: Janet Opal Jeppson
    to Isaac Asimov
    "
    Location:
    (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/Isaac_Asimov)
Children2

SignatureIsaac Asimov

Isaac Asimov (mnamo 2 Januari 1920 - 6 Aprili 1992) alikuwa mwandishi wa bunilizi ya kisayansi nchini Marekani. Alikuwa pia mtaalamu wa biokemia mwenye PhD kutoka

Maisha

Asimov alizaliwa huko Petrovichi, Smolensk, Urusi katika familia ya Kiyahudi. Tarehe ya kuzaliwa haijulikani, ilitokea kati ya 4 Oktoba 1919 na 2 Januari 1920. Alisheherekea sikukuu yake kwenye 2 Januari. Wazazi walihama Marekani pamoja naye alipokuwa na umri wa miaka 3. Alijifunza lugha za Kiyiddish na Kiingereza tangu utotoni.

Alisoma kemia kwenye Chuo Kikuu cha Columbia akahitimu shahada ya uzamili kwenye mwaka 1941 akaendelea kupokea digrii ya uzamivu (PhD) mnamo 1948. Wakati huohuo aliandika pia masimulizi na vitabu. Tangu 1951 alikuwa profesa kwenye Chuo Kikuu cha Boston ilhali aliendelea kuandika.

Baada ya mafanikio ya kitabu chake The Naked Sun (1957) aliacha kazi ya kisayansi akaendelea kutunga vitabu vyake.

Aliandika vitabu vingi, hasa masimulizi na riwaya juu ya ustaarabu ujao ambako watu huishi pamoja na roboti yaani mashine zenye uwezo wa kufikiri zinazopewa maumbile ya kufanana na binadamu.

Asimov alitunga pia vitabu vinavyoeleza sayansi kwa watu waskio wataalamu alikuwa mshauri wa kisayansi kwa filamu za Star Trek zilizotengenezwa kwa runinga.

Maandishi

Isaac Asimov 
Daftari ya Tyrann (1951) ya senti 25

Vitabu vya Asimov's vilivyokuwa mashuhuri zaidi vilikuwa vitabu vya mfululizo wa Foundation series. Aliandika pia Galactic Empire na Robot Series. Kwa jumla alitunga au alihariri zaidi ya vitabu 500 akaandika barua 90,000 letters. Pamoja na bunilizi ya kisayansi aliandika pia kuhusu sayansi yenyewe, historia, Biblia, fasihi na

Maandishi mengi ya mapema ya Asimov yalikuwa hadithi fupi zilizochapishwa katika majarida na daftari za hadithi za bei rahisi. Miaka baadaye, yalikusanywa na kuchapishwa tena kama makusanyo. Mikusanyiko inayojulikana ni pamoja na I, Robot, The Rest of the Robots, Earth is Room Enough na The Early Asimov.

Orodha ya Asimov

Asimov alitunga orodha ya vitabu vyake 15, akishauri visomwe kwa utaratibu huu:

    1. I, Robot (1950). baadaye The Complete Robot (1982).
    2. Caves of Steel (1954).
    3. The Naked Sun (1957).
    4. The Robots of Dawn (1983).
    5. Robots and Empire (1985).
    6. The Currents of Space (1952).
    7. The Stars, Like Dust (1951).
    8. Pebble in the Sky (1950).
    9. Prelude to Foundation (1988).
    10. Forward the Foundation (1993).
    11. Foundation (1951).
    12. Foundation and Empire (1952).
    13. Second Foundation (1953).
    14. Foundation's Edge (1982).
    15. Foundation and Earth (1986).

1-5 ni vitabu vya 'Roboti'; 6-8 ni vitabu vya 'Galacticos Empire'; 9-15 ni vitabu vya mfululizo wa Foundation .

Riwaya za Asimov zimeathiri bunilizi ya kiayansi kwenye runinga na sinema. Hasa 'Three Laws of Robotics' (kanuni tatu za uroboti) zilichangia kwenye majadiliano ya kimataifa kuhusu teknolojia hiyo.

  1. Roboti haiwezi kumdhuru mwanadamu au, kwa kutotenda, kumruhusu mwanadamu aje ajeruhi.
  2. Roboti inapaswa kutii maagizo yoyote ambayo wanadamu wamepewa, isipokuwa pale ambapo maagizo hayo yatapingana na Sheria ya Kwanza.
  3. Roboti lazima ilinde uwepo wake maadamu ulinzi huo haugongani na Sheria ya Kwanza au ya Pili.

Imani

Ingawa alizaliwa katika familia ya Kiyahudi, Asimov alijiita kafiri anayekana Mungu:

    "Mimi ni kafiri kabisa. Ilinichukua muda mrefu kusema hiyo. Nimekuwa mtu asiyeamini Mungu kwa miaka mingi, lakini kwa namna fulani ... ilikuwa afadhali kusema ni humanisti au mtu asiyejua kama Mungu yupo au la."

Kifo

Alipofanyiwa upasuaji wa moyo mnamo 1983, alipokea damu iliyoambukizwa VVU. Alipata UKIMWI, akafa kutokana na athari za hali ya kiafya mnamo 1992.

Marejeo

Viungo vya Nje

Isaac Asimov 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
Isaac Asimov 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Isaac Asimov  Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Isaac Asimov kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Isaac Asimov MaishaIsaac Asimov MaandishiIsaac Asimov ImaniIsaac Asimov KifoIsaac Asimov MarejeoIsaac Asimov Viungo vya NjeIsaac Asimov

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

DakuMaghaniMachweoNgekewaMfumo katika sokaLady Jay DeeLahaja za KiswahiliBaruaDubai (mji)Madawa ya kulevyaSabatoMbogaAzimio la kaziMweziKinembe (anatomia)TenziBara la AntaktikiJinaHifadhi ya mazingiraMkoa wa SimiyuMartin LutherNdoa katika UislamuOrodha ya miji ya Afrika KusiniSimbaKukuFigoKamusi Hai ya Kiswahili MtandaoniHoma ya manjanoMaji kujaa na kupwaHektariHali ya hewaFutiTungo kiraiTanganyika African National UnionKifua kikuuTitanicPemba (kisiwa)HadithiUmoja wa Muungano wa AfrikaMarekaniTovutiMamaTetekuwangaTarbiaKiswahiliWairaqwUpendoRupie ya Afrika ya Mashariki ya KijerumaniMawasilianoUfufuko wa YesuNominoBabeliUtataMuungano wa Tanganyika na ZanzibarMsamiatiMaji ya chumviWasukumaJulius NyerereSintaksiWajitaDhima ya fasihi katika maishaDoto Mashaka BitekoJumuiya ya nchi zinazozalisha mafuta dunianiMwakaNgeli za nominoNyongoUkooUpinde wa mvuaEe Mungu Nguvu YetuMuundoHuduma ya kwanzaIsraelMapambano ya uhuru TanganyikaFonolojia🡆 More