Hassi (hassium) ni elementi ya kikemia iliyo na alama Hs na namba atomia 108. Hassi ni yenye dutu nururifu; isotopi iliyo thabiti zaidi ni 269 Hs, ikiwa na nusumaisha ya takriban sekunde 16.
Hassi (hassium) | |
---|---|
Jina la Elementi | Hassi (hassium) |
Alama | Hs |
Namba atomia | 108 |
Mfululizo safu | Metali ya mpito |
Uzani atomia | 265, 269, 270 |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 32, 14, 2 |
Densiti | 41 g/cm³ (kadirio) |
Ugumu (Mohs) | (haijulikani) |
Asilimia za ganda la dunia | 0 % (elementi sintetiki) |
Hali maada | inaaminiwa ni mango |
Mengineyo | tamburania, nururifu |
Hassi ni elementi sintetiki ambayo haipatikani kiasili; inaweza kutengenezwa kwa viwango vidogo kwenye maabara.
Majaribio ya kwanza ya kusanidi elementi 108 zilifanywa katika maabara ya Dubna, Moscow Oblast, kwenye Umoja wa Kisovyeti, mnamo 1978. Hatimaye wanasayansi katika taasisi ya utafiti wa ioni nzito huko Darmstadt, Ujerumani, waliweza kuonyesha kwamba walifaulu kuitengeneza.
Kwa hiyo wanasayansi Wajerumani walipewa nafasi ya kuchagua jina la elementi mpya wakachagua jina hassium kutokana na Hesse, moja ya majimbo 16 ya shirikisho la Ujerumani.
Hakuna habari nyingi kuhusu tabia za Hessi maana inaweza kutengenezwa tu kwenye maabara kwa viwango vya gramu lakini kwa gharama kubwa, na baada ya kutengenezwa haidumu maana atomu zake zinaachana haraka.
|url-access=
ignored (help)This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Hassi, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.