Embe

Embe ni tunda tamu na lenye vitamini nyingi litokalo katika mti wa mwembe, aina mbalimbali za spishi Mangifera indica.

Embe
Maembe
Embe
Maembe mtini
Embe
Bilauri ya juisi ya maembe.

Likiwa na asili ya Asia Kusini, kwa sasa ni kati ya miti ya kitropiki inayokuzwa kwa matunda yake yanayoweza kuliwa na yanayovunwa sana duniani, hususan katika tropiki.

Pamoja na kuliwa bichi, embe pia hutumika katika mapishi mbalimbali na kwa kutengenezea juisi.

Maelezo

Zaidi ya spishi hizi zinapatikana kwa maumbile kama miembe ya porini. Jenasi ni sehemu ya familia ya korosho, Anacardiaceae. Miembe inatoka Asia ya Kusini ambapo “Mwembe wa Kihindi” au “mwembe wa kawaida,” Mangifera indica, ulisambazwa duniani ukaanza kuwa tunda moja la yanayopandwa zaidi ya dunia. Spishi nyingine za Mangifera (kama mwembe wa farasi, Mangifera foetida, n.k.) zinakuzwa kwa misingi midogo. Ulimwenguni, kuna mamia ya aina za mwembe. Kulingana na aina, ukubwa, sura, utamu, rangi ya ganda, na rangi ya nyama zinatofautiana. Mwili wa tunda unaweza kuwa na rangi ya njano, ya dhahabu, au ya machungwa. Embe ni tunda la kitaifa la Uhindi na la Pakistan, na mwembe ni mti wa kitaifa wa Bangladesh.

Miembe hukua urefu hadi mita 35-40. Miti hiyo inaishi kwa muda mrefu sana na mifano fulani inatoa bado matunda baada ya miaka mia tatu. Katika udongo wenye kina, mzizi mkuu unaenda mita sita chini ya uso, na mizizi ya kulisha na ya kushikilia inapenyapenya vipana. Majani ni kibichi kila wakati. Ni sentimita 15-35 kwa urefu na sentimita 6-16 kwa upana. Majani yanapokuwa madogo, yana rangi ya machungwa na ya waridi. Yanabadilika kuwa mekundu, kisha kijani yanapokomaa. Maua yanatengenezwa kwa vikundi juu ya shina, sentimita 10-40 kwa urefu. Kila ua ni jeupe na lina petali tano za 5-10 milimita kwa urefu.

Matunda yaliyoiva yanatofautiana kwa sura, ukubwa, rangi, utamu, na ubora wa kula. Kulingana na aina, tunda ina rangi ya njano, ya machungwa, ya kijani, au nyekundu. Tunda lina mbegu moja haijitenga kutoka kwenye nyama kwa urahisi. Tunda linaweza kuwa na urefu wa sentimeta 5-25 na masi ya 140 gramu mpaka 2 kilogramu.

Kilimo

Maembe yamekuzwa katika Asia ya Kusini kwa maelfu ya miaka na yaliwahi katika Asia ya Kusini Mashariki kati ya karne ya nne na karne ya tano KYK. Kufikia karne ya kumi BK, kilimo chake ameanza huko Afrika ya Mashariki. Msafiri Mmoroko Ibn Battuta aliripoti uwepo wake mjini Mogadishu. Kilimo chake kilienea Brazil, Bermuda, Karibiani, na Meksiko, ambapo hali ya hewa inaruhusu ukuaji wake.

Kwa sasa, embe linakuzwa katika zaidi ya mazingira ya kitropiki na sub-tropiki yenye joto. Karibu nusu ya maembe ulimwenguni yanatoka Uhindi tu, na chanzo kikubwa cha pili ni Uchina.

Matumizi ya upishi

Maembe kwa kawaida huwa na ladha tamu, lakini ladha na umbile la nyama vinatofautiana kadili ya aina. Ganda la embe lisiloiva, lililopikwa, na lililovundika inaweza kulewa, lakini inaweza kuwasha kinywa. Maembe hutumiwa sana jikoni. Embe kali lisiloiva, linatumiwa kwa mchuzi na achari, au linaliwa mabichi na chumvi au pilipili moto. Lassi ni kinywaji maarafu sana katika Asia ya Kusini, kinachoandaliwa na kuchanganya embe lililoiva na mgando na sukari. Matumizi ya embe ya kawaida zaidi ni kuliwa bichi baada kuiva, litakapokuwa na ladha nzuri inayopendeza sana.

Tanbihi

Marejeo

  • Ensminger, Audrey H. (1995). The Concise Encyclopedia of Foods & Nutrition. CRC Press. uk. 651. ISBN 0-8493-4455-7. 
  • Litz, Richard E. (editor, 2009). The Mango: Botany, Production and Uses. 2nd edition. CABI. ISBN|978-1-84593-489-7.
  • Susser, Allen (2001). The Great Mango Book: A Guide with Recipes. Ten Speed Press. ISBN|978-1-58008-204-4.

Viungo vya nje

Embe 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
Embe  Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Embe kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Embe MaelezoEmbe KilimoEmbe Matumizi ya upishiEmbe TanbihiEmbe MarejeoEmbe Viungo vya njeEmbeMtiMwembeSpishiTundaVitamini

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

ShuleWamasoniJiografia ya TanzaniaKaaOsama bin LadenUbongoMnyoo-matumbo MkubwaNileUtandawaziKanisa KatolikiAbedi Amani KarumeBiasharaUturukiMaadiliMishipa ya damuStephane Aziz KiBiashara ya watumwaKiwakilishi nafsiMwanga wa JuaViwakilishi vya kumilikiLeopold II wa UbelgijiYerusalemuTarakilishiTanganyika African National UnionMaghaniNdiziNgonjeraOrodha ya nchi za Afrika kulingana na idadi ya watuKamusi ya Kiswahili sanifuDiplomasiaMohammed Gulam DewjiKoloniOrodha ya mikoa ya Tanzania na Pato la TaifaPaul MakondaKanuni ya Imani ya Nisea-KonstantinopoliHistoria ya WokovuVita ya Maji MajiKylian MbappéMichoro ya KondoaAsiliWayao (Tanzania)JinsiaBinadamuVivumishiKongoshoUkooHistoria ya Kanisa KatolikiNgeliHali ya hewaIsraeli ya KaleNyotaHadhiraUpinde wa mvuaMajiKunguniDar es SalaamNgano (hadithi)UjimaVichekeshoWilaya za TanzaniaPasifikiOrodha ya Marais wa BurundiOlduvai GorgeNevaTungo kishaziMwenge wa UhuruShinaPichaHafidh AmeirEmmanuel John NchimbiKifua kikuuUandishiNafsiNdege (mnyama)MariooKiunguliaRejistaDawa za mfadhaiko🡆 More