Demi Gene Guynes (amezaliwa tar.
11 Novemba 1962) anafahamika kwa jina la kikazi kama Demi Moore, ni mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani.
Demi Moore | |
---|---|
Demi Moore mnamo 2010 | |
Amezaliwa | Demi Gene Guynes 11 Novemba 1962 Roswell, New Mexico, US |
Kazi yake | Mwigizaji |
Miaka ya kazi | 1982–hadi sasa |
Ndoa | Freddy Moore (1982–1985) Bruce Willis (1987–2000) Ashton Kutcher (2005–2013) |
Baada ya nyusika ndogondogo katika filamu na maigizo ya vipindi vya televisheni General Hospital, Moore amekuza kazi yake katika filamu kama vile St. Elmo's Fire (1985) na Ghost (1990) na mwanzoni mwa miaka ya 1990 amekuwa miongoni mwa waigizaji wa kike wenye kulipwa mapesa mengi sana katika Hollywood kwa kufuatia mafanikio yake katika filamu kama vile A Few Good Men (1992), Indecent Proposal (1993) Disclosure (1994). The Hunchback of Notre Dame (1996) na G.I. Jane (1997). Mwishoni mwa miaka ya 1990 filamu zake zilikuwa na mafanikio machache, lakini amerudi tena katika umaarufu na uhusika wake katika Charlie's Angels: Full Throttle (2003).
Moore amechukua jina lake la kikazi kutoka kwa mume wake wa kwanza Freddy Moore na ni mama wa watoto watatu kutoka katika ndoa yake na Bruce Willis. Baada ya kuolewa na mwigizaji Ashton Kutcher mwaka 2005 alibadili jina lake la mwisho kuwa Kutcher mnamo 2009.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani wa Marekani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Demi Moore kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Demi Moore, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.