Bahari ya Kaspi (Kiarabu: بحر قزوين Baḥr Qazvin; Kiajemi: دريا خزر darya khazar; Kirusi: Каспийское море kaspiiskoye more) ni ziwa kubwa kabisa duniani lenye eneo la km² 371,000 na mjao wa km³ 78,200.
Liko kati ya Azerbaijan, Urusi, Kazakhstan, Turkmenistan na Uajemi.
Kimo chake kinafikia mita 1,025.
Huitwa "bahari" kwa sababu maji yake ni ya chumvi ingawa si kali sana kama ya bahari yenyewe.
Upande wa kaskazini inaingia mito miwili mikubwa ya Volga na Ural. Inasababisha kiasi kidogo cha chumvi upande huo wa kaskazini. Asilimia ya chumvi huonegezeka kuelekea kusini.
Chini ya bahari kuna akiba kubwa za mafuta ya petroli na gesi, hasa karibu na Baku. Katika hori ya Kara-Bogas chumvi hulimwa.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Bahari ya Kaspi, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.