Ubaguzi wa rangi ni kitendo cha kuthamini au kutenga binadamu kwa misingi ya rangi za ngozi.
Ubaguzi wa rangi ulikuwa maarufu sana katika nchi kama Afrika Kusini kwa jina la "apartheid" na Marekani kwa jina la "segregation" ambapo huko Waafrika walikandamizwa kutokana na rangi yao katika kupata huduma mbalimbali za kijamii na kimaendeleo.
Wakati wa ukoloni, rangi ilitumika kama msingi wa utoaji huduma muhimu mfano: shule, matibabu na haki nyingine za kibinadamu. Rangi nyeusi ilipewa hadhi ya chini zaidi.
Siku hizi katika karibu nchi zote, sheria zinapinga ubaguzi wa rangi. Lakini katika nchi nyingi bado kuna wabaguzi wachache ambao wanavunja sheria kwa kuendelea kubagua. Kwa mfano, kuna wabaguzi wanaobagua Watu weusi nchini Marekani, nchini China, nchini India na katika nchi za Ulaya.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Ubaguzi wa rangi, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.