Armenia

Armenia (kwa Kiarmenia: Հայաստան Hayastan au Հայք Hayq) ni nchi ya mpakani kati ya Ulaya na Asia katika milima ya Kaukasi iliyoko kati ya Bahari Nyeusi na Bahari ya Kaspi.

Armenia


Armenia

Imepakana na Uturuki, Georgia, Azerbaijan na Iran. Upande wa kusini kuna eneo la nje la Kiazerbaijan linaloitwa Nakhichevan.

Ingawa kijiografia Armenia huhesabiwa mara nyingi kama sehemu ya Asia, kiutamaduni na kihistoria huhesabiwa pia kama sehemu ya Ulaya.

Jiografia

Mlima wa kitaifa wa Armenia ni mlima Ararat unaoaminika kuwa mahali ambako safina ya Nuhu ilikuta nchi kavu baada ya gharika kuu inayosimuliwa katika Biblia.

Historia

Armenia ni kati ya mataifa ya kale kabisa duniani, ingawa eneo lake limebadilika sana na eneo la sasa ni sehemu ndogo tu ya maeneo yaliyokuwa ya Armenia katika karne na milenia za nyuma.

Armenia ilikuwa nchi ya kwanza ya kupokea Ukristo kama dini rasmi ya kitaifa mnamo mwaka 301. Hadi leo karibu 93% za Waarmenia ni Wakristo wa Kanisa la kitaifa ambalo ni mojawapo kati ya Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki.

Jambo hilo lilichangia sana mateso yaliyowapata kutoka kwa majirani ambao wengi wao ni Waislamu, hasa Waturuki waliotawala kwa karne nyingi maeneo makubwa ya Dola la Osmani hadi Afrika na Ulaya.

Kilele chake kilikuwa maangamizi ya Waarmenia wakati wa vita vya kwanza vya dunia, ambapo waliuawa zaidi ya milioni moja.

Armenia ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti tangu 1920, ikapata uhuru wake tena mwaka 1991.

Kuna fitina na nchi jirani ya Azerbaijan kuhusu eneo la Nagorno-Karabakh linalokaliwa na Waarmenia lakini ni sehemu ya Azerbaijan kisiasa. Mipaka hii ni urithi wa zamani za Umoja wa Kisovyeti. Mara mbili kulikuwa na vita kati ya nchi hizo mbili. Hali halisi Armenia inatawala eneo hili ingawa Nagorno Karabakh ilijitangaza kuwa jamhuri ya kujitegemea isiyokubaliwa na umma wa kimataifa.

Watu

Wakazi ni hasa Waarmenia asilia (98.1%), halafu Wayazidi (1.2%), Warusi (0.4%) n.k.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kiarmenia, ambacho kina alfabeti ya pekee iliyobuniwa na mtakatifu Mesrop mwaka 405 BK.

Upande wa dini, mbali ya Kanisa la kitaifa (92.5%), Wakristo wengine (Waprotestanti na Wakatoliki) ni asilimia 2.3 za wakazi na Wayazidi wanaofuata dini yao asili ni asilimia 0.8.

Matunzio ya picha

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Armenia 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Armenia  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Armenia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Armenia  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Armenia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Armenia JiografiaArmenia HistoriaArmenia WatuArmenia Matunzio ya pichaArmenia Tazama piaArmenia MarejeoArmenia Viungo vya njeArmeniaAsiaBahari NyeusiBahari ya KaspiKaukasiKiarmeniaUlaya

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

MuhammadUraibuOrodha ya vitabu vya BibliaDemokrasiaVieleziMwanzo (Biblia)FonetikiWiki FoundationJiniLugha rasmiSan Jose, CaliforniaSimbaDubuUainishaji wa kisayansiKiarabuBiasharaLugha za KibantuMorokoWanyaturuUzazi wa mpango kwa njia asiliaMkoa wa SimiyuMadhehebuMaambukizi nyemeleziMwanamkeAfrika ya Mashariki ya KijerumaniLongitudoMange KimambiZuchuUnyevuangaUsawa (hisabati)MadiniChelseaJuxMeta PlatformsDar es SalaamLimauHussein KaziMaambukizi ya njia za mkojoDawatiMaji kujaa na kupwaEthiopiaUbunifuVivumishi vya pekeeBomu la nyukliaMaskiniSerikaliMkoa wa RukwaCristiano RonaldoAngahewaViwakilishi vya pekeeKipindupinduWilaya ya NyamaganaInsha ya wasifuMungu ibariki AfrikaLil WayneJamhuri ya Watu wa ZanzibarChuiHistoria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoSteven KanumbaBilioniWagogoBabuAmina ChifupaBenki ya DuniaVivumishi vya kumilikiMweziUkimwiAkiliMoyoAfyaTungoSayariFasihi andishiMkoa wa KigomaTambikoBinadamuUtata🡆 More