Sataranji

Sataranji (kutoka Kiajemi/Kiarabu شطرنج shatranj; pia: chesi kutoka Kiingereza chess) ni mchezo wa ubao kwa wachezaji wawili.

Sataranji
Ubao wa chesi kabla ya kuanza mchezo; saa zatumiwa wakati wa mashindano anbapo kila mchezaji anapewa muda fulani tu.

Ubao wa sataranji

Ubao wa sataranji huwa na umbo la mraba na ndani yake kuna miraba midogo 64 inayobadilishana kwa rangi nyeupe na nyeusi. Kuna pia badiliko la rangi za kahawia nyeupe na kahawia nyeusi au rangi mbalimbali.

Kete za sataranji

Jina la kete Herufi ya kifupi Picha
Shaha, kete kuu
K (King)
Sataranji Sataranji 
Malkia
Q (Queen)
Sataranji Sataranji 
Ngome
R (Rook)
Sataranji Sataranji 
Sataranja
B (Bishop)
Sataranji Sataranji 
Farasi
N (Knight)
Sataranji Sataranji 
Kitunda
P (Pawn)
Sataranji Sataranji 

Kila mchezaji huwa na kete 16 zinazopangwa kwa namna maalumu ambayo ni sawa kwa kila upande na kila safari. Isipokuwa zinatofautiana kwa rangi, kwa hiyo kuna mchezaji mweupe na mchezaji mweusi. Mweupe huanza mchezo; safari inayofuata wachezaji wanabadilishana rangi.

Kete ni za aina mbili:

  • vitunda vinane ambavyo ni kete zenye nguvu ndogo zinasimamishwa kwenye mstari wa pili mbele ya mchezaji. Vitunda vyote ni sawa, hakuna tofauti kati ya kitunda na kitunda.
  • kete 8 za juu ambazo ni ngome 2, farasi 2, sataranja 2, malkia 1 na mfalme 1.

Kete za juu zinapangwa kwa namna ifuatayo: ngome -farasi -sataranja -malkia -shaha -sataranja -farasi -ngome.

Mchezo

Mchezo huanzishwa na mchezaji mwenye kete nyeupe anayehamisha kete ya kwanza jinsi anavyoamua. Halafu zamu ya mwenye kete nyeusi hufuata na mchezo unaendelea kwa zamu.

Kila kete ina mwendo wake wa pekee. Kete haiwezi kuhamia mraba wenye kete ya rangi yake. Lakini ikimaliza mwendo wake kwenye mraba wenye kete ya rangi nyingine inaikamata maana yake kuiondoa kutoka ubaoni na kuchukua nafasi yake kwenye mraba. Kete iliyokamatwa hairudi tena: ni kama imefungwa au kufa.

Katika mwendo wake kete haiwezi kupita juu ya miraba yenye kete nyingine isipokuwa kete ya farasi ambayo ina uwezo wa kuruka. Vinginevyo mwendo ama unakwisha mbele ya kete nyingine au inaweza kuikamata na kuchukua nafasi yake.

Sataranji 
Mwisho: Shaha nyeusi ameshindwa; hana mahali anapoweza kwenda bila kutishiwa tena.

Shabaha ya mchezo ni ushindi. Ushindi unapatikana kama kete ya shaha inatishwa moja kwa moja na kete nyingine ilhali haina nafasi ya kuhamia mahali pasipo tishio. Shaha haiwezi kukamatwa; ikiweza kushambuliwa bila mahali pa kukimbilia, mchezo unakwisha. Hali hii huitwa kwa lugha nyingi "mat" ambalo ni neno la Kiajemi linalomaanisha "amekwisha, hawezi". Kwa Kiingereza ni "checkmate".

Mwendo

Sataranji 
Kuanzia upande wa kushoto hapo kuna shaha mweupe, ngome nyeusi, malkia mweusi, kitunda cheupe, farasi nyeusi na sataranja nyeupe.

Shaha Shaha ni kete kuu katika mchezo; inatembea hatua 1 (=mraba 1) kila upande. Kuna hatua ya pekee ambayo ni kuruka ngome.

Malkia

Ngome

Sataranja

Farasi

Kitunda
Kete ya Kitunda hutembea mbele bila kunyoka tu hadi mwisho wa ubao. Mwendo wake ni hatua ya mraba mmoja. Lakini hatua yake ya kwanza kama haijatembea bado ina nafasi ya kutembea hatua mbili za mraba. Mara nyingi mchezaji mwenye kete nyeupe huanza mchezo kwa kusukuma kitunda kilichopo mbele ya shaha.

Kitunda kikitembea mbele hakina uwezo wa kukamata kete ya adui iliyopo mbele yake. Kituda hukamata kete iliyopo upande wa kushoto au kulia wa mraba mbele yake.

Kama kitunda kinafikia mstari wa mwisho wa ubao kinaondolewa na kubadilishwa kwa kete nyingine yoyote isipokuwa kete kuu ya shaha. Badiliko la kitunda huwa ni uamuzi wa mchezaji wake.

Tanbihi

Viungo vya Nje

Sataranji  Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Sataranji kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Sataranji Ubao wa sataranjiSataranji Kete za sataranjiSataranji MchezoSataranji MwendoSataranji TanbihiSataranji Viungo vya NjeSataranjiKiajemiKiarabuKiingerezaMchezoUbao

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Utawala wa Kijiji - TanzaniaRais wa Afrika KusiniMitume na Manabii katika UislamuKumaBajetiSilabiViwakilishi vya unganifuShengMsituJamaikaHistoria ya KanisaUzazi wa mpango kwa njia asiliaMwenge wa UhuruWilaya za TanzaniaMjombaMkoa wa TaboraVidonda vya tumboMapinduzi ya ZanzibarNadhariaSimbaHifadhi ya mazingiraUandishi wa barua ya simuMunguUajemiUtumwaWaziri wa Mambo ya Ndani (Tanzania)Orodha ya Marais wa UgandaElimuKiambishi tamatiVivumishi ya kuulizaWapareMishipa ya damuKitenzi kikuu kisaidiziWazaramoWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiUmaskiniVivumishi vya kumilikiMandhariDiraMadiha AbdallaRasiYoung Africans S.C.HisiaOrodha ya Magavana wa TanganyikaMkoa wa IringaMazingiraMchwaUkomeshaji wa Biashara ya WatumwaLughaKichochoMbuga za Taifa la TanzaniaLongitudoCaliforniaUenezi wa KiswahiliKinuShomari KapombeNdege (mnyama)VatikaniDoto Mashaka BitekoWanyamweziOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaMauaji ya kimbari ya RwandaTiktokTendo la ndoaHistoria ya UislamuMshororoUdhibiti wa sarataniHussein Ali MwinyiHali ya hewaMachweoNamba tasaReli ya Tanganyika🡆 More