Uturuki: Nchi katika Ulaya Kusini-Mashariki na Asia Magharibi

Uturuki (Jamhuri ya Uturuki; kwa Kituruki: Türkiye Cumhuriyeti) ni nchi ya kimabara kati ya Asia na Ulaya.

Uturuki

Sehemu kubwa iko Asia ya magharibi lakini sehemu ndogo ya eneo lake upande wa magharibi wa Bosporus iko Ulaya.

Jiografia

Uturuki: Jiografia, Historia, Nchi ya kisasa 
Ramani ya Uturuki

Sehemu kubwa ya mipaka yake ni bahari: Mediteranea upande wa magharibi na kusini na Bahari Nyeusi upande wa kaskazini. Kwenye nchi kavu imepakana na Ugiriki na Bulgaria upande wa magharibi, Kaskazini-mashariki na Georgia, Armenia na Azerbaijan, kwa upande wa mashariki na Iran na upande wa kusini na Iraq na Syria.

Sehemu kubwa ya eneo lake ni Anatolia inayoonekana kama rasi kubwa kati ya Mediteranea na Bahari Nyeusi. Hali ya nchi ndani ya Anatolia mara nyingi ni yabisi na kilimo kinategemea umwagiliaji.

Safu za milima zinafuatana na pwani za kusini na kaskazini.

Sehemu ya mashariki ya nchi kuelekea Uajemi na Kaukazi ina milima mingi.

Maeneo ya pwani yanapokea mvua na huwa na rutuba.

Historia

Waturuki waliwahi kuwa kiini cha Milki ya Osmani iliyounganisha mataifa mengi chini ya Sultani wa Konstantinopoli.

Uturuki wa kisasa umetokea kama nchi ya pekee baada ya vita viwili mwanzoni mwa karne ya 20.

Jamhuri ya Uturuki ilianzishwa mwaka 1923 na jenerali Kemal Atatürk baada ya vita vikuu vya kwanza, vilivyomalizika kwa kuvunja Milki ya Osmani, na vita vilivyofuata, vya kuondoa wanajeshi wa Ugiriki na nchi nyingine walioingia ndani ya sehemu iliyokuwa imebaki baada ya kuvunjika kwa dola kubwa.

Atatürk alileta mabadiliko mengi yaliyolenga kuondoa utamaduni wa kale wa Waosmani na enzi za utawala wa sultani wa Kiislamu.

Magharibi ya nchi imeendelea sana lakini maeneo ya mashariki yamebaki nyuma.

Nchi ya kisasa

Siku hizi Uturuki unalenga kuingia katika Umoja wa Ulaya.

Serikali ina utaratibu wa kidemokrasia ya vyama vingi. Utawala wa nchi ni kwa mikoa 81.

Mji mkuu ni Ankara ulioko katika kitovu cha Anatolia.

Mji mkubwa ni Istanbul ulioitwa zamani Konstantinopoli na zamani zaidi Bizanti: ulikuwa mji mkuu wa Dola la Uturuki hadi mwaka 1923.

Wakazi

Uturuki una wakazi zaidi ya milioni 76. Wengi wao (70-75%) ni Waturuki.

Katika mashariki ya Uturuki watu wengi ni Wakurdi ambao ni milioni 14 au takriban 20% za raia wote wa Uturuki.

Kuna mabaki madogo tu ya Wagiriki na Waarmenia waliowahi kukalia sehemu kubwa za nchi hadi mwisho wa milki ya Osmani.

Kwenye maeneo jirani na Syria wako pia Waarabu.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kituruki, kinachotimika na 85% za wakazi. Hata hivyo, lugha 36 huzungumzwa nchini Uturuki, yaani 14 za asili na 22 za nje (angalia orodha ya lugha za Uturuki).

Upande wa dini, karibu wote ni Waislamu, hasa kuanzia karne ya 20 ambapo Wakristo wengi waliuawa (hasa Waarmenia) au kuhama (hasa Wagiriki). Waliobaki ni 0.2% tu. Hata hivyo Uturuki ni nchi isiyo na dini rasmi.

Picha za Uturuki

Tazama pia

Viungo vya nje

Uturuki: Jiografia, Historia, Nchi ya kisasa 
WikiMedia Commons
Wiki Commons ina media kuhusu:
    Jumla
    Serikali
    Utalii
    Uchumi
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Uturuki: Jiografia, Historia, Nchi ya kisasa  Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Uturuki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Uturuki JiografiaUturuki HistoriaUturuki Nchi ya kisasaUturuki WakaziUturuki Picha za Uturuki Tazama piaUturuki Viungo vya njeUturukiAsiaKiturukiNchi ya kimabaraUlaya

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Khadija KopaMwenge wa UhuruMkoa wa MaraHistoria ya KanisaDolar ya MarekaniIstilahiShirika la Utangazaji TanzaniaWajitaKaswendeMkoa wa DodomaNyumba ya MunguMoshi (mji)Orodha ya Vyuo Vikuu vya TanzaniaJamhuri ya Kidemokrasia ya KongoVladimir PutinUzazi wa mpango kwa njia asiliaUislamuIbadaAgano JipyaReal MadridKisaweBunge la TanzaniaMmeaSamakiBiasharaMtawaNamba ya mnyamaMbuga za Taifa la TanzaniaMajira ya baridiMfumo wa vyama vingiLigi Kuu Uingereza (EPL)Paul MakondaTanganyika (ziwa)NdiziChristina ShushoPanziJuxMbwana SamattaMagonjwa ya machoMatiniMamaSanaa za maoneshoManchester CityUtapiamloUmoja wa AfrikaKataDhima ya fasihi katika maishaNomino za dhahaniaMartha MwaipajaIsimujamiiLuka ModricNomino za jumlaMkoa wa ShinyangaMkoa wa MtwaraInshaKamusiElizabeth MichaelHoma ya matumboMaishaMbuJiografia ya TanzaniaKunguniMadhehebuZanzibar (Jiji)Moses KulolaSentensiKamusi za KiswahiliMagonjwa ya kukuTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya TanzaniaUchawiEthiopia🡆 More