Liechtenstein

Utemi wa Liechtenstein (kwa Kijerumani: Fürstentum Liechtenstein) ni nchi ndogo katika Ulaya ya Kati.

Imepakana na Uswisi na Austria. Ni ya sita kati ya nchi huru ndogo zaidi duniani.

Liechtenstein

Mji mkuu ni Vaduz wanapoishi wakazi 5000.

Liechtenstein
Ramani ya Liechtenstein

Jiografia

Nchi yote ina urefu wa km 24.56& kutoka kaskazini hadi kusini na upana wa km 12.36.

Urefu huu unafuata mwendo wa mto Rhine ambao ni mto pekee nchini, pia ni mpaka na Uswisi.

Upande wa mashariki na karibu na mpaka wa Austria milima hupanda hadi kimo cha mita 2,599.

Historia

Kwa muda mrefu nchi ilikuwa sehemu ya Dola Takatifu la Kiroma ingawa chini ya utawala wa kikabaila.

Dola hilo liliposambaratishwa na Napoleon Bonaparte (1806), Liechtenstein ilijiunga na Shirikisho la Rhein hadi mwaka 1813 ambapo lilifutwa, halafu na Shirikisho la Ujerumani (1815-1866).

Ndipo ilipopata uhuru kamili ikitegemea ulinzi kutoka Uswisi.

Uchumi

Lichtenstein imekuwa nchi tajiri baada ya vita kuu ya pili ya dunia kwa sababu serikali ya mtemi ilidai kodi ndogo kabisa zilizohamasisha makampuni mengi ya nje kufungua ofisi zao nchini.

Kuna pia benki nyingi zinazosemekana kuficha pesa za matajiri ambao wangetakiwa kulipa kodi ya mapato nyumbani kwao.

Siasa

Mkuu wa nchi ni mtemi Hans-Adam II anayeitwa kwa jina kamili "Johannes „Hans“ Adam II Ferdinand Alois Josef Maria Marko d'Aviano Pius von und zu Liechtenstein". Tangu tarehe 15 Agosti 2004 amemkabidhi mwanawe Alois madaraka ya utawala.

Bunge la wabunge 25 huchaguliwa na wananchi wote. Sheria zote zinapaswa kukubaliwa na mtemi. Mawaziri watano wa serikali huteuliwa na bunge na kuthibitishwa na mtemi. Wananchi wote wana haki ya kupeleka mapendekezo ya sheria, au kudai kura ya wananchi wote juu ya sheria iliyopitishwa na bunge na kuthibitishwa na mtemi.

Watu

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kijerumani.

Upande wa dini, wakazi wengi ni Wakristo, hasa Wakatoliki (78.4%) na Wakalvini (7.9%).

Michezo

Tangu 1984 Liechtenstein imejiunga na FIFA na UEFA na inashiriki tangu 1994 katika uteuzi wa timu za soka katika mashindano ya kombe la Ulaya na kombe la dunia.

Hata kama nchi ya wakazi 37,000 tu, na haina klabu mashuhuri, Waliechtensetin waliweza kushtusha wapinzani wao mara kadhaa.

Mwaka 1996 klabu ya Vaduz ilishinda klabu ya Latvia FC Universitate Riga 1–1 na 4–2 lakini ilishindwa baadaye na Paris St. Germain.

Timu ya taifa ya 2004 iliweza kumaliziana na Ureno 2–2 na kushinda Luxemburg 4-0.

Tazama pia

Liechtenstein  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Liechtenstein kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Tags:

Liechtenstein JiografiaLiechtenstein HistoriaLiechtenstein UchumiLiechtenstein SiasaLiechtenstein WatuLiechtenstein MichezoLiechtenstein Tazama piaLiechtensteinAustriaKijerumaniNchi huruUlaya ya KatiUswisi

🔥 Trending searches on Wiki Kiswahili:

Kamusi elezoBurundiKukuKitenzi kikuu kisaidiziKaswendeMkoa wa SongweJangwaZiwa ViktoriaKinjikitile NgwaleKylian MbappéNyati wa AfrikaKima (mnyama)Jiografia ya TanzaniaPepopundaWikipediaHaki za watotoImaniFacebookZuchuHekalu la YerusalemuNamba tasaMichezoLugha ya kwanzaUyahudiUkristo nchi kwa nchiJipuKichochoNgw'anamalundiKamusiEmmanuel John NchimbiHistoria ya IsraelUfupishoArusha (mji)ElimuPunyetoKifua kikuuMajiKomaJamhuri ya Watu wa ZanzibarUkoloniOrodha ya Magavana wa TanganyikaKichecheTarafaMwanga wa JuaMfumo wa upumuajiBahatiUvimbe wa koromeo usababishwao na streptokokiUgonjwa wa kuharaWimbo wa Jumuiya ya Afrika MasharikiOrodha ya Marais wa MarekaniDubai (mji)Mkoa wa ManyaraHifadhi ya SerengetiKongoshoUhuru wa TanganyikaWimboNambaUturukiNetiboliMzunguBibliaHifadhi ya mazingiraJeshi la Ulinzi la Wananchi wa TanzaniaMsamiatiMkoa wa IringaNomino za kawaidaMohammed Gulam DewjiLugha za KibantuTasifidaIniOrodha ya Marais wa UgandaMagonjwa ya kukuDiplomasiaTamthilia🡆 More