Kitenzi ni istilahi ya sarufi kwa maneno yanayotaja matendo kama vile kufanya, kwenda, kulala, kupiga, kuishi na kadhalika.
Mifano |
---|
|
Lugha nyingi zinatumia vitenzi ingawa kuna pia lugha zisizoweka tofauti kati ya vitenzi na majina.
Kwa Kiswahili kila kitenzi kina shina lake linalobeba maana yake. Mfano: ku-fanya ambamo "fanya" ni shina; kiambishi awali "ku-" ni alama ya aina ya neno yaani kitenzi chenyewe.
Ndani ya shina kuna tofauti kati ya mzizi wa neno "fany" na kiambishi tamati ambacho ni silabi "a".
Mzizi wa kitenzi wenyewe haubadiliki wakati wowote kitenzi kinaponyambuliwa katika kauli yoyote iwayo.
Vitenzi kwa Kiswahili hupokea viambishi mbalimbali vinavyoeleza kwa undani zaidi maana ya matumizi ya neno. Viambishi awali ni silabi zilizopo mbele ya mzizi na viambishi tamati ni silabi zilivyopo baada ya mzizi wa kitenzi.
Viambishi awali vinaweza kutaja:
Viambishi tamati vinaweza kupanua au kubadilisha maana ya msingi ya mzizi wa neno. Mifano ni kimbi-a, kimbi-lia, kimbili-ana, kimbi-za, kimbi-zana, kimbi-liwa.
Kwa jumla kitenzi cha Kiswahili kinaweza kuwa na sehemu saba, yaani shina na hadi viambishi sita mbele au nyuma ya shina la neno. Jedwali linalofuata linaonyesha mifano kadhaa. Umbo fupi zaidi ya kitenzi ni amri kama "piga".
1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 |
---|---|---|---|---|---|---|
Viambishi awali | Shina | Viambishi tamati | ||||
Viambishi vya Nafsi Mtenda | Viambishi vya Wakati / Hali | Viambishi Virejeshi | Viambishi vya Nafsi Mtendewa | Viambishi vya Kauli | Kiishio | |
ni | na | - | - | sem | - | a |
u | me | ni | on | yesh | a | |
a | na | cho | ni | ambi | - | a |
tu | li | po | wa | ingi | z | a |
pig | - | a |
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kitenzi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article Kitenzi, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.