K ni herufi ya 11 katika katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa.
Alfabeti ya Kilatini (kwa matumizi ya Kiswahili) | ||||||
---|---|---|---|---|---|---|
Aa | Bb | Cc | ch | Dd | ||
Ee | Ff | Gg | Hh | Ii | Jj | |
Kk | Ll | Mm | Nn | Oo | Pp | |
Rr | Ss | Tt | Uu | Vv | ||
Ww | Xx | Yy | Zz |
Asili yake ni Kappa ya alfabeti ya Kigiriki.
Kisemiti asilia: picha ya kofi | Kifinisia: Kaf | Kigiriki: Kappa | Kietruski: K | Kilatini: K |
---|---|---|---|---|
Asili ya herufi K ni katika miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.
Wafinisia walikuwa na kaf iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya kofi (au: uso wa mkono) wakitumia alama tu kwa sauti ya "k" na kuiita kwa neno lao kwa kofi "kaf". Wagiriki walichukua alama hiyo na kuiita "kapha" bila kujali maana asilia ya "kofi" ilikuwa sauti tu ya "k".
Waitalia ya kwanza wakaendelea kutumia alama kwa aina ya "k". Waroma mwanzoni hawakutumia alama hii kwa sababu hawakuwa na "k" jinsi Waetruski walivyoitamka. Kwa sauti ya "k" ya kawaida Waroma walitumia C. Lakini baadaye baada ya Roma kutwaa na kutawala Ugiriki walianza kutumia maneno mengi ya Kigiriki wakaingiza K ya Kigiriki katika alfabeti yao wakaitumia wka maneno ya kigeni tu.
This article uses material from the Wikipedia Kiswahili article K, which is released under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 3.0 license ("CC BY-SA 3.0"); additional terms may apply (view authors). Maudhui yanapatikana kwa chini ya CC BY-SA 4.0 isipokuwa iwe imebainishwa vinginevyo. Images, videos and audio are available under their respective licenses.
®Wikipedia is a registered trademark of the Wiki Foundation, Inc. Wiki Kiswahili (DUHOCTRUNGQUOC.VN) is an independent company and has no affiliation with Wiki Foundation.